BAISKELI ILIVYOKATISHA MAISHA YA BOSI TANESCO
NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Mhandisi Boniface Gissima Nyamohanga, pamoja na dereva wake, Muhajiri Mohammed Haule, waliopoteza maisha katika ajali ya barabarani iliyotokea usiku wa kuamkia jana katika eneo la Bunda, mkoani Mara.











