DK.BITEKO ATAKA MIGOGORO IEPUKWE
NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko amewataka wanajamii kujiepusha na mazingira yanayoweza kusababisha migogoro baada ya wao kufariki Dkt. Biteko amesema hayo jana Jijini Dar es Salaam alipomwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kufungua Kongamano na Mkutano Mkuu wa mwaka wa Chama cha Wanasheria Wanawake nchini (TAWLA).







