KAMPENI YA KISHERIA YA MAMA SAMIA
YAWAFIKIA WATANZANIA MILIONI 43
NA MWANDISHI WETU, ARUSHA
KAMPENI ya Msaada wa Kisheria ya Mama Samia Legal Aid ikiwa ikiwafikia Watanzania Milioni 43 hatimaye imetua jiji la Kitalii Arusha, ambapo wakazi wake wamehamasishwa kujitokeza ili kutoa kero zao.Wananchi hao wameahidiwa kutatuliwa migogoro mbalimbali inayowasumbua kwa muda mrefu ambapo wanasheria kupitia kampeni hiyo wataanza kusikiliza na kutafuta utatuzi kwa siku 10 mfululizo.







