KATIKA kile kile kinachoonekana kujiimarisha zaidi katika uwekezaji Serikali ya Zanzibar, imejipanga kuweka mazingira mazuri zaidi katika uwekezaji visiwani humo.
Hii yote ni kuhakikisha wakazi wa Zanzibar na Watanzania kwa ujumla wanafaidika na matunda ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo yalikuwa na lengo la kumtoa mwananchji waka waida katika ukandamizaji na unyonyaji.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la seMapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amethibitisha hilo na kusema Zanzibar itaendelea kuweka mazingira mazuri zaidi ya kuwavutia wawekezaji zaidi ya uwekezaji hapa nchini.
Rais Dkt. Mwinyi alitoa hakikisho hilo hivi karibuni, wakati alipozungumza na Balozi wa Tanzania nchini, Celestine Kakele aliyefika Ikulu kujitambulisha.
Kutoa hakikisho hilo, Rais Dkt. Mwinyi ameeleza kuwa kuna fursa kubwa ya nchi hizo mbili kushirikiana hasa katika Sekta ya Utalii na Uwekezaji ambazo zikifanyika vyema nchi hizo zinaweza kunufaika kwa kiasi kikubwa.
Dk. Mwinyi amemsisitiza Balozi Kakele kufanya juhudi maalum za kuwavutia wawekezaji kutoka Nigeria kuja kuangalia fursa za Uwekezaji na Serikali inaandaa Mazingira mazuri ya kuwa na Uwekezaji wenye tija na Endelevu.
Ame muhakikishia Balozi huyo kuwa Serikali inaimarisha Uwekezaji kwa kuondoa vikwazo vinavyozorotesha ushirikiano kwa lengo la kuwavutia wawekezaji.