TUNAPOZUNGUMZIA ujasiriamali ni lazima kwanza ujue nini maana ya neno hilo ambalo lilianza kutumika miaka ya 1700 likiwa na maana ya kawaida ya kuanzisha biashara.
Lakini maana ya ujasiriamali kutoka kwa wachumi, ujasiriamali ni kukabiliana na vikwazo za biashara endapo kuna uwezekano wa kupata faida. Kwa wengine ni kuwa na uwezo wa kukwepa vikwazo za biashara ili ufanikishe biashara yenye faida.
Pia wengine wamemuelezea mjasiriamali kama ni mtu mbunifu mwenye uwezo wa kuuza ubunifu wake. Wachumi wengine wameendelea kumuelezea mjasiriamali kama mtu mwenye kuleta bidhaa au huduma za kibunifu kwenye soko ambazo hazijawahi kuwepo.
Katika karne ya 20, mchumi mmoja kwa jina Joseph Schumpeter (1883- 1950) alifafanua kuwa mjasiriamali ni mtu mwenye kuleta ubunifu na maboresho yenye kuleta sio tu hamasa bali pia kuwa kichocheo cha mabadiliko.
Joseph Schumpeter aliendelea kumuelezea mjasiriamali kama “mbunifu mharibifu” maana yake ni kwa kuwepo wajasiriamali na bidhaa au huduma zake, viwanda huduma na au bidhaa dhaifu na za zamani zilikufa na kutoweka kabisa kwenye soko.
Wachumi wengi leo hii wanaamini kuwa mjasiriamali ni moyo na kichocheo katika kukua kwa chumi za nchi mbalimbali duniani.
Lakini maana ya ujasiriamali kutoka kwa wafanyabiashara ilifafanuliwa na Peter Drucker (1909-2005) alielezea wazo hili kwa mapana mengine kuwa, mjasiriamali ni mtu anayepeleleza mabadiliko, kuwa na mwitikio wa haraka na kuhatamia fursa zilizopo katika mabadiliko. Mfano wa hili ni mabadiliko yaliyotokea katika sekta ya mawasiliano kutoka typewriter kwenda kompyuta.
Mjasiriamali anaweza kutokea katika hali yeyote, msomi au sio msomi, mhandisi, mwanasheria au mwalimu mchungaji.
Lakinimjasiriamali huyu anaweza akawa anataka kukopa na akawa anashindwa ajue wapi pa kuanzia, hivyo ni vyema pia ukazijua mbinu tano ambazo unaweza kuzitumia katika kuhakikisha unapata mkopo benki.
Fahamu benki ni mkopeshaji mkubwa na mgumu kwa mazingira ya Tanzania. Pamoja na hayo benki wana masharti maalumu ambayo nayo hutofautiana kulingana na nani anakopa, anakopa kiasi gani na kwa ajili ya biashara ipi na soko lipi. Kila benki inaweza kuwa na vigezo tofautotofauti.
Mikopo mikubwa huambatana na masharti lukuki tofauti na mikopo midogo. Mikopo kwa watu wenye rekodi nzuri ya kulipa ni tofauti na mkopo kwa watu wenye rekodi mbaya au ambao ndio kwanza wanaomba mkopo kwa mara ya kwanza.
Mkopo kwa watu maarufu au makampuni yenye majina ni tofauti kwa watu wasio maarufu au taasisi zisizo na majina.
Ebu tuangalie dondoo hizi hapa chini zitakazokusaidia kujua masharti muhimu ya mabenki:
1.Je ni biashara mpya au inayoendelea? Biashara inayoendelea na yenye angalau miaka mitatu ina nafasi kubwa kuliko zile changa au mpya
2. Aina ya biashara unayofanya Biashara za kuzalisha zinanafasi kubwa kuliko zile za huduma au uchuuzi
3. Integrity (historia safi ) ya mkopaji Historia safi ya mkopaji ya kukopa na kurudisha bila usumbufu inaongeza uwezekano mkubwa wa kupewa mkopo
4. Dhamana na mdhamini wa mkopaji kama akishindwa kurudisha Kw a b a h a t i m b a y a m k o p a j i akishindwa kurudisha kwa namna yeyote ile mkopo, je kitu gani kitafidia huo mkopo ili benki wasipate hasara au nani atasimama kama mdhamini ili yeye ndie ashikwe endapo mkopaji atashindwa kurudisha mkopo. Aina ya dhamana na mdhamini atakayekubaliwa na benki itasaidia wewe kupata mkopo
5. Mchanganuo wa Biashara Mchanganuo wa biashara wenye kuonyesha mchanganuo wa kisekta, ushindani, uzalishaji, uongozi/utawala, masoko na mambo ya fedha kwenye fedha hasa mtaji utakaohitajika, makisio ya mauzo, gharama, na faida. pia makisio ya balance sheet na cashflow itatakiwa.
Hii ni pamoja na uwiano wa sehemu muhimu za biashara kama uwiano wa mauzo na matumizi, mauzo na mishahara, mauzo na mtaji, mauzoi na gharama ghafi, muda wa kurudisha gharama na kuanza kupata faida na mengineyo