TUMBUSI ni ndege w a k u b w a w a mawindo wa familia ya Accipitridae na Carthatidae. Tumbusi ni ndege wanaokula mizoga hasa katika maeneo ya hifadhi za wanyama na katika maeneo yenye mashamba ya wanyama.
Ndege hawa huweza kupatikana katika maeneo ya hifadhi za wanyamapori na wakati mwingine hupatikana nje ya hifadhi. Upatikani huu hutegemea na upatikanaji wa vitu muhimu kama chakula, sehemu ya kuzalia na kuishi. Tumbusi kama ndege wengine wakubwa, huruka kwa kusaidia na (thermals).
Hivyo hutegemea jua linapotoka liwasaidie kupaa na hawarushi mabawa (vultures don’t flap) yao kama ndege wengine hivyo kupaa juu sana. Maumbile ya tumbusi yamewawezesha kuwa na uoni wa hali ya juu. Tumbusi anadhaniwa kuona hadi mita 1000 akiwa angani na hii huwasaidia katika kuona sehemu zenye mizoga na kusanyiko la tumbusi wengine.
Spishi nyingi za Tumbusi hazina manyoya kichwani, sifa hii huwasaidia wasichafuke na damu wakati wa kula mizoga. Endapo kungekuwa na manyoya kichwani angepata shida wakati wa kupasua na kula mizoga.
Hivyo, kukosekana manyoya kichwani husaidia urahisi wa kujisafisha anapofika sehemu zenye maji. Tumbusi wapo kwenye hatari ya kutoweka kwa vile idadi yao imekua ikupungua kwa kasi sana katika maeneo yao ya asili.
Kati ya matishio ya kutoweka kwao ni sumu inayotumika kwa kukusudia kuua tumbusi ili kuficha matendo ya ujagili na kwa imani potofu za kishirikina au kwa makusudio ya kulipiza mauaji ya wanyama wengine kama Simba wanaoua mifugo ya jamii za karibu na hifadhi.
Njia nyingine ya sumu ni matumizi ya viwatilifu visivyo salama kutibu w a n y a m a – n a t u m b u s i wanapokula mizoga yao hufa. Kulingana utafiti uliofanywa na shirika lisilo la serikali la Nature Tanzania katika Jumuiya ya Usimamizi wa Wanyamapori yaani Wildlife Management Area (WMA), unaonyesha idadi ya tumbusi Ndege Tumbusi; ‘Sabuni ya Mazingira’ inayoangamizwa imekua ikipungua kwa kiasi kutokana na kuuawa kwa sumu. Baada ya kuuwa wananchi hao hutumia viuongo vya tumbusi kwa ajili ya tiza za asili.
FAIDA ZA NDEGE TUMBUSI Ni muhimu kujua faida ambazo ndege hawa wanatupatia katika mifumo mbalimbali ya kiikoloji( mazingira) lakini pia kiuchumu kama ifuatavyo; Ndege hawa wana jukumu muhimu la kula mizoga na hivyo kusaidia kudhibiti magonjwa mfano Kimeta.
Uwepo wa Tumbusi ni Kiashiria muhimu cha afya ya mfumo wa ikolojia. Kwa kuzingatia ongezo mkubwa la wanyamapori, tumbusi huonyesha afya ya mfumo wa ikolojia Tumbusi wanaweza kuwa viashiria muhimu vya shughuli za ujangili kwa vile wanavutiwa na mizoga mikubwa, kama ile ya tembo na vifaru waliowindwa Tumbusi wanaweza kuthibitisha kuwa kiashiria muhimu cha mafanikio ya uhifadhi linapokuja suala la ongezeko lao.
Lakini pia ndege hawa ni kivutio kikubwa cha utalii kwani watalii hutoka kwenye mataifa ya kigeni na hata wale watalii wa ndani huenda katika hifadhi zetu za taifa kwa ajili ya kuwaangalia ndege hawa. Kwa hiyo uhifadhi wa ndege tumbusi kikamilifu utalisaidia taifa letu la Tanzania kujipatia fedha za kigeni.
Ndege hawa hutumika katika kufanya tafiti za kisayansi. Zipo faida zaidi hizo hapo juu na tumbusi ni muhimu waendelee kuwepo na kuongezeka kwani kukosekana kwao kuna madhara makubwa yanaweza kutokea. Ili kujenga uelewa zaidi soma kisa hiki ambacho kilitokea nchini india baada ya Tumbusi kutoweka.
India kunakadiriwa kusababisha hasara ya karibu Dola bilioni 34 kutokana na ongezeko la mbwa mwitu. kufuatia kupungua kwa tumbusi ambao walisababisha milipuko ya kichaa cha mbwa na hvyo kuleta madhara kwa mbwa na na wanadamu. Ni vyema jamii kushirikiana na asasi za kiraia na mashirika binafsi katika uhifadhi wa ndege hawa kwani wana faida nyingi katika mazingira hadi kufikia kuitwa “sabuni ya mazingira”.
Usiache kutoa taarifa kwenye mamlaka zinazohusika na uhifadhi wa wanyamapori juu ya watu wanaosababisha vifo vya ndege hawa. Lakini pia kuacha kuweka sumu kwenye mizoga kwani ni hatari kwa ndege hawa wala mizoga na uwekaji wa sumu ni kunyume cha sheria kwa mujibu wa sheria ya uhifadhi wa wanyamapori Tanzania ya mwaka 2022 na sheria ya mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori Tanzania ya mwaka 2013 adhabu kali hutolewa kwa anayeshikwa akitumia sumu kwa lengo la kuua wanyamapori