MAONO na maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan yamewezesha kufanyika kwa kikao muhimu na chenye tija, kati ya Serikali na Wizara ya Viwanda na Biashara ili kujadili changamoto mbalimbali na kuzipatia utatuzi.
Kikao hicho kilichoelekezwa na Rais Dkt. Samia kilikutanisha uongozi wa Serikali chini ya wizara hiyo na kushirikisha ule wa Shirikisho la Sekta Binafsi Tanzania (TPSF) ili kujadili mambo mbalimbali.
Mazungumzo hayo yalisongozwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda na Biashara Dkt. Hashil Abdallah ambapo alisema kimefanyika kwa maelekezo ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kukaa, kukutana na kujadili mambo yote yanayorahisisha shughuli za ufanyaji biashara nchini.
Dkt. Abdallah amesema katika majadiliano hayo wamepanga kufanya vikao endelevu na kuazimia kufanyika kwa mkutano mkubwa wa kisekta, MPPD, ambapo utakuja kufanya majumuisho yaliyojadiliwa katika mkutano huo.
Ametoa pongezi kwa shirikisho hilo kwa kuboresha sera zao na muundo unaoendana na falsafa za Awamu ya Sita na kwa kufanya hivyo Serikali itakuwa bega kwa bega na Shirikisho hilo kwani wamedhihirisha kuwa sekta hiyo inabadilika kulingana na mazingira ya Mifumo ya Biashara.
Naye Mwenyekiti wa Shirikisho hilo Angelina Ngalula amesema kuna mabadiliko wameyafanya kwenye uendeshaji wa taasisi ili kuweza kutoa mchango mkubwa kwa Serikali katika kuimariaha uchumi wa nchi.
A m e s e m a m a b a d i l i k o h a y o yamefanywa kwenye nyanja za teknolojia, masuala ya kidigitali, wafanyabiashara wadogo, vijana, afya, elimu na mabadiliko ya tabia ya nchi pamoja na kujumuisha taasisi na Mabaraza ya Wilaya ili kutatua kero na kujenga uelewa wa mipango ya Shirikisho na mifumo.
Ameishukuru Wizara na Taasisi zake kwa ushirikiano kati yao ambao umeboresha utendaji k azi wa Shirikisho kuliko miaka minne iliyopita ambayo ilikuwa na malalamiko makubwa hasa kwenye tozo pamoja na kuanza mapema maandalizi ya Maonesho ya OSAKA-EXPO nchini Japan.