NA MWANDISHI WETU
JONATHAN Ikangalombo winga hatari wa Yanga aliyesajiliwa kutoka AS Vita kutoka nchini DRC, ambaye Jangwani wanamwita ‘Mashine ya Kugusa na Kuachia’ atatambulishwa rasmi kwa mashabiki pia ataanza kuichezea timu hiyo dhidi Gopco FC katika mchezo wa Kombe la ASFA, mchezo utakaopigwa kwenye Uwanja wa KMC Mwenge Jijini Dar es salaam.
Nyota huyo aliyesajiliwa katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo anatajwa kuwa ni moto wa kutolea mbali anayeweza kuwakumbusha mashabiki wa timu hiyo makali ya aliyekuwa winga teleza wa Jangwani, Tuisila Kisinda.
“Huyu ana kasi zaidi ya Tuisila Kisinda lakini tofauti yeye ana uwezo wa kuingia kati na ana jicho la kupachika mabao kama ilivyokuwa kwa Fiston Mayele” alisema kiongozi mmoja wa Yanga aliuyeshuhudia nyota huyo akijifua, hata hivyo hakutaka jina lake liandikwe gazetini.
Yanga ambayo wiki iliyopita iliwaomba radhi mashabiki wake kutokana na kushindwa kuvuka kihunzi kucheza hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika, sasa imawataka waendelee kuwa karibu nao, wakianza kuewasha moto katika mchezo huo ambao utawashuhudia wachezaji wao wakitoa burudani ya nguvu.