NA ILHAM JUMA
MWENYEKITI mstaafu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Freeman Mbowe amesema uchaguzi wa viongozi ndani ya chama hicho umeacha majeraha mengi miongoni mwa wanachama.
Kufuatia hali hiyo, Mbowe ameshauri viongozi walioingia madarakani kukiponya chama hicho kutokana na majeraha hayo.
Amesema yeye aliahidi angeshinda nafasi ya Uenyekiti angeunda Tume ya Ukweli na Upatanishi ili watu wakazungumze yaliyojiri kuelekea uchaguzi huo ambapo pale watu walipokoseana adabu, walipokosa nidhamu, walipokosa maadili, walipokibagaza chama hicho wakasameheane, wapeane mikono ili CHADEMA ikawe yenye nguvu zaidi.
Mbowe ameyasema jana katika Ukumbi wa Mikutano wa Mlimani City, Dar es Salaam baada ya kutangazwa kwa matokeo ya uchaguzi wa viongozi wa kitaifa wa chama hicho.
“Ni kweli tumefanya uchaguzi jana hadi leo uliokuwa huru, wa wazi, wa haki ambayo kila binadamu mwenye akili timamu ameiona. Uchaguzi kuwa huru, wa haki, na wa wazi halipaswi kuwa tukio la siku moja, linapaswa kuwa mchakato wote unaojenga hadi siku ya kesho”,
“Nimesema mara nyingi na ninasema tena, kwa namna ambavyo wagombea mbalimbali na mashabiki wao walivyojinasibu katika kujen