NA ASHA SEKEFU
WACHEZAJI Simba wametoa yao ya moyoni na kusema, kufanikiwa kutinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, huku wakiongoza kundi lao kumeifanya timu hiyo izidi kuogopwa zaidi barani Afrika.
Akizungumza kwa niaba yao, Nahodha wa Simba, Mohammed Hussein `Zimbwe Jr’, amesema kumaliza kinara wa kundi kwenye michuano kombe la Shirikisho Afrika kumewapa nafasi ya kumewafanya wazidi kuwa tishio barani Afrika.
Simba hatua inayofuata ya robo fainali inatarajiwa kucheza na kati ya Stellenbosch ya Afika Kusini, Al Masry ya Misri au Asec Mimosa ya Ivory Coast.
“Kwa Level
ya Simba ilipofikia sio kuogopa timu au mpinzani yoyote anayekuja mbele yetu, siku zote unapomaliza nafasi ya juu unatengeneza nafasi ya mpinzani kukuogopa,” amesema.
Zimbwe Jr amesema baada ya kufanikiwa sasa wanahitaji kuona Simba inaendelea kufanya vizuri katika hatua inayofuata na kucheza nusu fainali.
“Simba bado haijawa imara kama ilivyokuwa misimu mitatu au minne, lakini taratibu tunarudi kwenye ubora wetu kwa kuwa tishio kwa mashindano ya ndani na nje,” amesema.