Mkurugenzi mkuu wa WHO Dkt. Tedros Ghebreyesus Leo kwenye mkutano na vyombo vya habari ikulu chamwino, maeeleza mchango wa shirika la afya duniani kwa Tanzania dhidi kupambana na ugonjwa wa Marburg.
Kwenye mkutano huo akiwa na mwenyeji wake Raisi Dkt. Samia Suluhu Dkt. Tedros amesema WHO itaendelea kuiunga mkono Tanzania katika kukabiliana na kudhibiti mlipuko wa virusi hivyo.
Aidha Dkt. Tedros amesema jitihada za Serikali katika kukabiliana na mlipuko uliotokea mwaka 2023 zimeijengea uwezo ambao unaiwezesha Tanzania kuudhibiti kwa uharaka mlipuko uliotokea hivi sasa.
Vilevile, Dkt. Tedros amempongeza Rais Dkt. Samia kwa kujidhatiti kwake katika huduma ya afya kwa wote kupitia kutunga Sheria ya Bima ya Afya kwa Wote ya mwaka 2023.