Natafakari juu ya miaka takribani 50 iliyopita, watu walivyokuwa wanaishi katika wakati huo, hakukua na umeme wala maji safi, hakukua na miundombinu bora kwaajili ya maendeleo, hata upatikanaji wa chakula ulikuwa wa shida.
Je! Unakumbuka safari ya kutoka mwanza mpaka Dar es Salaam ilichukua takribani siku saba hadi nane, Umesahau kuhusu maji ya kunywa tulishirikiana na wanyama kwenye visima, kwani ww haukujifunza ukiwa chini ya mti kufata kivuli na vipi kuhusu kuwahi kula na kulala kwasababu kibatari/Chemli inakaribia kuzima kwa kukosa mafuta, Vipi pilau mpaka sikuku na baiskeli nyingi kuliko magari?.
Ni kumbukumbu tuu ambazo zinanifanya niumie ila nisijutie kuwepo kwa wakombozi wa maendeleo yetu kwasababu bila wao sijui tungelikuwa wapi sasa.
Sidhani kama kuna mwamba anaweza kusimama na kuituhumu siasa kama anajua mchango wa siasa nchini, nilianza na kuku kumbusha juu ya tulipotoka kisha uniambie bila siasa tungekuwa hapa?
Msingi wa maendeleo nchini ni chama tawala. Je! Unatambua utofauti wa CCM na vyama vya upinzani?
Katika mikutano inayofanywa na CCM yanazungumzwa mambo mengi lakini ukifika wakati wa ilani na sera za chama cha mapinduzi hapa ndipo utofauti wa CCM na vyama vya upinzani unapoanzia.
Maendeleo na ukuaji wa taifa vipo chini ya chama tawala hivyo basi mara zote hufikiria kupambana na changamoto za wananchi ili kukuza uchumi wa nchi na wananchi na sio kupambana na wapinzani tuu.
Aliesema kila mtu hutafuta asichokua nacho hakukosea hata kidogo.
Chama cha mapinduzi mara zote huwaza juu ya kusaidia watanzania lakini vyama vingine vinawaza kushinda uchaguzi na kuwa na mikakati mingi ya uchaguzi na kushika dola kuliko maendeleo ya nchi. Huu ndio ukweli.
Ili update majibu ya hili fatilia ajenda za mikutano ya vyama vya upinzani nchini mara nyingi ni mikakati ya kushinda uchaguguzi kuimarisha chama na kushika dola. Lakini kwa CCM hujadili ajenda za chama na maendeleo ya taifa bila kutenganisha.
Sizungumzii ilani ‘hapana’ nazungumzia ajenda za vikao na mikutano, ilani inaweza kuwepo kwenye chama ili kionekane bora kwenye uchaguzi lakini mafanikio hupatikana katika mikakati ya mara kwa mara kama ambavyo CCM inafanya kujadili maendeleo kwenye vikao vyao mara kwamara kulinganisha na vyama pinzani.
Hiyo nitofauti ya CCM na vyama vya upinzani.