Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu amemshukuru kinana kwa kwa wakati wake wote aliokitumika chama cha mapinduzi na kuwa kada muaminifu, mtiifu na mzalendo wa chama.
Aidha amemshukuru kwa kutumikia serikali katika nafasi tofauti tofauti kwa uadilifu mkubwa huku akiainisha nafasi alizotumikia ni pamoja na jeshi la wananchi na kuwa waziri wa ulinzi nchini.
Vilevile akieleza ni wakati wake kinana sasa wakupumzika baada ya kukitumikia chama cha mapinduzi kwa muda mrefu katika nafasi tofauti tofauti ikiwemo kuwa mjumbe wa halmashauri, katibu mkuu wa chama cha mapinduzi na makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi bara.