mkutano mkuu wa chama cha mapinduzi unaofanyika Leo tarehe 18 Januari 2025 jijini dodoma, ni mkutano wa kihistoria wenye mambo mengi ya kujenga Tanzania mpya na kuimarisha chama cha mapinduzi (CCM)
mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka ndani na nje ya taifa la Tanzania, watu mashuhuri, wasanii, wajumbe wa chama na wanachama wa CCM vikiwemo vyama vya kisiasa kutoka katika mataifa ya nchi jirani ikiwemo chama cha Ferlimo kutoka nchini msumbiji
Aidha mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wastaafu, wakuu wa mikoa na wilaya, mawaziri na viongozi wa asasi mbalimbali za kijamii na taasisi za serikali
Vilevile jumla ya waliohudhuria mkutano huo ni watu zaidi ya (5000) huku ndani ya ukumbi wakiwa ni watu elfu tatu (3000) na nje ya ukumbi kwenye mahema maalumu ni watu elfu mbili (2000)