KWA mujibu wa taarifa iliyotolewa na Klabu ya Yanga ni kwamba beki wake wa kushoto Yao Kouassi, hatukuwa miungoni mwa wachezaji watakaotumika katika kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa MC Alger mchana wa Jumamosi, katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa kwenye Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salsaam.
Kouassi ni miungoni mwa mabeki wazoefu kikosini atakuwa nje kutokana na kufanyiwa upasuaji utakaomuweka nje ya uwanja kwa takriban wiki nne, huku beki mkongwe ndani ya kikosi hicho Kibwana Shomari akipewa majuku ya kuvaa viatu vyake.
Shomari aliyedumua ndani ya kikosi cha Yanga kwa muda mrefu, bado anaitumikia timu hiyo hadi mwaka 2026 ambapo katika mechi za hivi karibuni alionyesha uwezo mkubwa katika nafasi yake ya beki wa kushoto aliyokuwa akicheza Yao Kouassi.
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe aliwatoa hofu mashabiki akisema kuwa hakutakuwa na peno katika mchezo huo muhimu utakaoiwezesha timu hiyo ya Wananchi kushinda na kutinga hatua ya Robo Fainali ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika.