KHA! Bosi wa zamani wa timu ya England na Manchester City, Sven-Goran Eriksson ‘amefuatwa kaburini na deni’ la Paundi milioni 8 (Sh bilioni 24.5) na sasa nyumba yake imewekwa sokoni ili kufidia deni hilo.
Eriksson ambaye alifariki dunia Agosti mwaka jana kwa tatizo la saratani na sasa, haya yanaonekana kama malipo kwake ya kumsindikiza ‘kaburini’ kwa kuibuliwa kwa deni hilo.
Kuibuka kwa deni hilo kwa kocha huyo mkongwe, ilionyesha alikopa fedha hizo kabla ya mauti kumkutaTambapo aliweka dhamana nyumba yake inayopigwa mnada.
Lakini nyumba yake inayotakiwa kupigwa mnada ina thamani ya Paundi milioni 3.8 (zaidi ya Shilingi bilioni 11) na kitendo cha kuuzwa kwake imeonekana kuwafadhaisha wengi.