NA MWANDISHI WETU
KUSOGEZWA mbele kwa fainali za Kombe la Mataifa Afrika kwa Wachezaji wa Ndani (CHAN) kulikofanywa na Shirikisho la Soka Afrika (CAF), kumeiibua Serikali iliyosema miezi sita inatosha kuweka miundo mbinu bora zaidi.
Hayo yalisemwa na Naibu Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma, aliyesema kuongezwa kwa miezi sita ya maandalizi inatoa nafasi kuendelea kuwa bora kwa miundo mbinu.
Kauli hiyo aliitoa jana, kwenye hafla ya Kongamanano la wadau wa Michezo kuelekea CHAN na fainali za AFCON 2027.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) Jumanne, juzi limetangaza kuahirishwa kwa michuano ya CHAN ambayo ilitakiwa kufanyika Februari 1 hadi 28 lakini sasa kusogezwa mbele hadi Agosti mwaka huu.
āTanzania tulikuwa tumefika kwa asilimia 90 ya maboresho ya uwanja na kuwa tayari kwa michuano hayo, lakini baada ya kupokea taarifa ya kusongezwa mbele kwa mashindano hayo inatoa muda wa kujipanga vizuri na mashindani hayo kuwa na utofauti na tulivyopanga,ā amesema.
Wakati huohuo, Serikali imewaomba wadau wa soka kuunga mkono timu ya taifa āTaifa Starsā katika maandalizi ya CHANā yatakayofanyika Agosti mwaka huu.
Agizo hilo limetolewa na Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko alipofungua Kongamano la wadau wa michezo kuelekea CHAN 2024 na AFCON 2027.
Dk. Biteko amesema wadau wanapaswa kuunga mkono maandalizi ya timu ya taifa ili ijiandaee vyema na michuano hiyo.
āWito kwa wadau wa soka na Watanzania kiujumla kuiunga mkono timu yetu ya taifa katika maandalizi ya CHAN, pamoja na kutoa rasilimali katika kuwezesha timu hiyo kipindi cha maandalizi,ā amesema.