Kongamano la wadau wa michezo kuelekea CHAN 2024 na AFCON 2027 lililofanyika Johari Rotana januari 15,2025 limeweka wazi juu ya ujio wa fursa nyingi zitakazo patikana wakati wa mashindano ambapo limesaidia kugusa wajasiriamali wote nchini katika kuzitambua fursa na kufanya ubunifu wao ili kusaidia kujenga mahusiano mazuri na wageni, pato lao na pato la taifa pia.
Kupitia taarifa ya utekelezaji wa maandalizi ya mashindano ya CHAN 2024 na kuelekea AFCON 2027 kwenye kongamano hilo zimeundwa kamati za kuhakikisha mashindano yanakwenda vyema lakini fursa zitakazo patikana zimewekwa wazi, fursa ambazo hazijawaaacha mbali wajasiriamali katika kufany a ubunifu wao kusaidia jamii kupata huduma na kutangaza pia utalii wetu kupitia vyakula na manzari nzuri za Tanzania.
Miongoni mwa kamati tatu(3) zilizoundwa kuhakikisha taratibu zinakwenda vyema katika mashindano hayo yanayotarajiwa kufanyika hivi karibuni ni Kamati kuu ya Kitaifa ambatyo kamati hii itayoongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kamati ya Wataalamu inayoundwa na Makatibu wakuu wote kutoka Wizara mbalimbali, Kamati hii itaongozwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu na kamati nyingine ni Kamati ya Kitaifa inayohusisha wadau kutoka sekta mbalimbali ambapo Kamati hii imejumuisha wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar na inayoongozwa na Ndg. Leodegar C.Tenga ambaye ni Mwenyekiti wa kamati hiyo.
Aidha Kwa mujibu wa taarifa ya utekelezaji wa maandalizi ya mashindano ya CHAN 2024 na kuelekea AFCON 2027, taarifa hiyo imeainisha baadhi ya maeneo wajasiriamali ambayo yamekidhi vigezo kutumika na CAF kipindi cha mashindano.
- Hoteli kwa malazi ya wageni mbalimbali zikiwemo Timu shiriki zimeainishwa na zimekidhi vigezo kutumika na CAF kipindi cha mashindano.Hoteli hizo ni Crown Plaza, Serena, Delta, Johari Rotana, Hyatt Regency, White sand na Lamada.
- Jamii imeshirikishwa katika kuhakikisha inashiriki ipasavyo wakati wote wa mashindano.
- Sekta binafsi zimeshirikishwa katika Kamati mbalimbali za mashindano ili kuhakikisha wanatumia fursa hii.
- Nafasi za Ajira pia zimetolewa kwa kipindi kifupi cha mashindano haya ya CHAN kuhakikisha vijana wanapata fursa (Volunteer).
Mahitaji yanayo hitajika katika mashindano ya chan 2024 na kuelekea afcon 2027 yanawasogeza wajasiriamali kufikia fursa mbalimbali wakati wa mashindano, miongonimwa mahitaji ni nyumba za wageni vyakula na mahitaji mengine kwa wageni.
Pia taarifa hiyo imeainisha faida zitakazo patikana kwa kuwa wenyeji wa mashindano hayo ikiwemo uhusiano wa kimataifa, fursa kwa wajasiriamali na wawekezaji nchini.
- Kuongezeka kwa uwekezaji na biashara kutokana na fursa za kutangaza nchi duniani kwa mashindano hayo;
- Ongezeko la wageni mbalimbali litafungua uchumi wa nchi hususan utalii
- Ajira za muda mfupi na mrefu wakati wa maandalizi na mashindano
- Kuimarika kwa huduma mbalimbali za jamii kama vile hoteli, nyumba za kulala wageni, migahawa.
- Masuala ya kidiplomasia yataimarika kutokana na ushirikiano wa nchi mbalimali
- Kuongezeka kwa pato la Taifa na Uchumi kwa mwananchi mmoja mmoja
Ni wakati wa kila mjasiriamali kuamka kufanya ubunifu kuelekea mashindano hayo ili kuweza kutatua matatizo, kutoa huduma, kuongeza kipato chao na pato la taifa pia kwani ni moja ya sifa za wajsiriamali wote ulimwenguni. Amka mjasiriamali ni wakati wa kuikimbilia fursa
.