Waziri wa zamani wa mambo ya ndani na kiongozi wa upimzani katika taifa la Bahari ya Hindi la Comoro apinga matokeo ya uchaguzi wa wabunge, ambao ulisusiwa na wapinzani, kwa tuhuma za udanganyifu.
Daud aliweka wazi kwamba wengi wa upimzani walikataa kushiriki katika uchaguzi huku kukiwa na madai kuwa kura ya raundi mbili ya kuwachagua wabunge 33 haikuwa na uwazi.
“Uchaguzi huo ulikumbwa na udanganyifu mkubwa, ujazo wa masanduku ya kura na katika vituo kadhaa, kulikuwa na kura nyingi zaidi ya waliojiandikisha,” alisema Daoud Abdallah.
Tume huru ya uchaguzi ya Anjouan, ilitangaza kuwa wagombea 12 kutoka chama tawala cha Convention for the Renewal of the Comoros (CRC) wameshinda.
Tume hiyo ilisema wagombea wa CRC walichukua kati ya asilimia 60 na 100 ya kura, huku waliojitokeza kupiga kura wakiwa asilimia 70.
Waziri anayesimamia uchaguzi, Fakridine Mahamoud, hakujibu maombi ya maoni kutoka kwa AFP.
Vilevile Assoumani, aliye madarakani tangu 2016, alikanusha shutuma za kujaza masanduku ya kura.”Si mara ya kwanza upinzani kukemea uchaguzi. Sasa, ni juu yao kuthibitisha shutuma zao,” alisema.
Duru ya pili ya upigaji kura katika taifa hilo inatarajiwa kufanyika Februari 16, ambapo Mohamed alisema wapinzani hawatashiriki “upinzani hautashiriki” .