- Ni Frank Mwalongo anayedaiwa kuyashawishi makampuni yaliyokopa mabilioni ya fedha benki kuacha kulipa mkopo yao na kukimbilia mahakamani kupata ushindi wa ‘kimkakati’
- Mahakama Kuu yapiga chini janja yake ya kutaka kampuni ya ZAS iliyokopa zaidi ya bilioni 20 kwa kampuni ya Lamar ya Dubai na kudhaminiwa na benki za Equity kenya na Tanzania isilipe mkopo huo
- Yaagiza ZAS Investiment Limited kuzilipa equity Kenya Dola milioni 5.6 na dola milioni 2.3 mtawalia
- Mahakama yaagiza pia kampuni hiyo illipe riba ya mkopo ya asilimia nane kuanzia tarehe ya kufungua madai hadi siku yah uku
- Wadau wapongeza mahakama kukataa kutumika kuhalalisha ‘wizi’ wa wazi wakisisitiza dawa ya deni ni kulipa
- Wamshangaa wakili anayewashauri ujinga wateja wake walioshindwa kulipa mikopo akiamini ataendelea kutumia udhaifu wa baadhi ya watendaji wa mahakama
- Kesi nyingine kadhaa za Mikopo CHECHEFU zinazosimamiwa na wakili huyo zinaendelea kuunguruma huku hukumu ya rufaa ya kesi ya NAS HAULIERS ikisubiliwa kwa hamu miezi kadhaa sasa
- Jamvi la Habari halifichi kitu
Na. Mwandishi wetu,
Usemi wa siku za mwizi arobaini na na mchuma janga hula na wakwao unaelekea kuendelea kumkuta wakili frank mwalongo anayedaiwa kuzunguka katika makampuni kadhaa ya wafanyabiashara wakubwa na wakati kuwashawishi waache kulipa marejesho ya mikopo waliyokopa na badala yake yeye kufungua kesi za kimkakati na kuwapatia ushindi makampuni hayo kuanza kugonga mwamba ama kuangukia pua baada ya juzi mahakama kuu divisheni ya biashara kuiamuru kampuni ya ZAS investment kuzilipa benki za Equity kenya na Tanzania mabilioni ya shilingi baada ya kushindwa kesi iliyofunguliwa nao kupitia wakili huyo aliyejaribu kutaka kuitumia mahakama kukwepa kulipa mikopo hiyo
Wakizungumza na gazeti hili mawakili Reuben Simwanza na Macdonald Lunyilija wamesema hakuna maana yoyote kwa wakili kuwashauri wateja wake waache kulipa mikopo badala yake kuheshimu makubaliano ya kisheria
‘’Jambo la wateja kukopa na kudefault malipo/marejesho ni jambo la kawaida kabisa, sio geni tunapokwenda mahakamani sio kwamba tunakwenda kubishana kuhusu kuchukua mkopo au kutokuchukua mkopo!! Tunakwenda kutafuta nafuu na kujaribu kuokoa dhamana iliyotumika tukiamini katika matarajio ya mteja kupata muda wa ziada kutazaa matunda kwa kupata ya kupata pesa na kurejesha mkopo wake’’. Amesema wakili Simwanza
‘’Mara nyingi wateja wa mtindo huo tunapowasikiliza na kuomba vielelezo tunaishia kuwashauri wakae chini kumalizana na benki lakini bahati mbaya saana unakuta maji yameshakorogeka (uvumilivu wa benki umeshindikana). Unakuta mteja kapatiwa kila nafuu ikiwa pamoja na restructuring ya mkopo husika kupata unafuu wa marejesho husika’’. Ameongeza
Wakili simwanza amesisitiza kuwa Kwa wateja waelewa na wenye mipango thabiti tunafanikiwa kufanya maelewano nje ya mahakama na wale wateja wagumu mnaishia kuendelea kuvutana mahakamani mkijaribu kupambana na ile mianya ya kiufundi zaidi kuliko kwenda kwenye merits/kiini cha mgogoro husika.
‘’ Binafsi naamini ili kuweza kuzilinda taasisi zetu za kifedha ili kuendelea kuwepo na kutoa huduma basi ni vyema kushauri wateja kurejesha mikopo yao na kuwakumbusha dawa ya deni ni kulipa sio kupoteza muda kwa kutumia milango ya mahakama’’. Amemalizia kusema wakili huyo wa mahakama kuu ya Tanzania
Kwa upande wake mwanasheria Macdonald Paschal,Wakili wa mahakama Kuu ya Zanzibar ameeleza ifuatavyo
‘’Kwa upande wangu nitoe rai kwa Pande zote za mkataba kwa kesi hii ni Mkopo wa Benki kuheshimu na kufuata makubaliano waliyoingia baina ya mkopeshaji na mkopaji. ‘’. Amesema Pascal
‘’Utaratibu wa makampuni Makubwa kukopa kwenye mabenki na kutofuata mikataba yao si kitu cha kujivunia kama nchi. Ni kweli makampuni haya hukimbilia Mahakamani Lakini imebainika Mara nyingi ni njia Yao ya kuchelewesha uwajibikaji kwenye mikataba ya mikopo waliyoingia na mabenki.’’. ameongeza
‘’Haki ya mkopeshaji kulipwa ipo palepale na hivyo baadaye Kupelekea usumbufu mkubwa zaidi kwa kukamatwa kwa mali za kampuni,akaunti zao kuzuiliwa na Kuuzwa kwa dhamana zilizowekwa kwa mkopeshaji’’. Amemalizia wakili huyo kijana
Kuhusu kesi hiyo, mapema jana gazeti maarufu nchini Tanzania la MWANANCHI kupitia mtandao wake wa www.mwananchi.co.tz iliripoti kwa kirefu kuhusiana kesi hiyo na hukumu yake
Katika taarifa yake mtandao huo umeripoti kuwa Kampuni ya ZAS Investment Company Limited imekwaa kisiki baada ya mipango yake ya kujaribu kukwepa kulipa deni la mkopo wa mabilioni ya fedha kutoka katika Benki za Equity Tanzania Limited na Equity Kenya Limited kunasa kwenye mtego wa Mahakama Kuu Divisheni ya Biashara.
Mahakama imeamuru kuwa kampuni hiyo ZAS ilikiuka mkataba wa mkopo wa kibenki uliosainiwa Oktoba 5, 2021.
Hivyo imeiamuru kampuni hiyo kuzilipa benki hizo deni la msingi la mkoopo huo jumla ya Dola za Marekani 8,064,807.88 (zaidi ya Dola 8.06 milioni) sawa na zaidi ya Sh21 bilioni.
Pia imeamuriwa kulipa riba ya compound ya asilimia nane ya kiasi hicho, kama ilivyobainishwa katika mkataba wa Oktoba 5, 2021, kuanzia tarehe ya kufungua madai kinzani mpaka, tarehe ya hukumu na riba ya asilimia saba kwa mwaka kuanzia tarehe ya hukumu mpaka tarehe ya kumalisha malipo yote.
Vilevile Mahakama imewaamuru wakurugenzi wake hao na kampuni hizo nyingine mbili kuzilipa benki hizo Dola za Markani 7,623,127.99 (zaidi ya Dola 7.6 milioni) sawa na zaidi ya Sh19.97 bilioni kama kiasi cha dhamana waliyoitoa kwa ZAS katika mkopo huo kwa kushindwa kutekeleza wajibu wao.
Mwisho kampuni hiyo na wadhamini wake wameamuriwa kulipa gharama za shauri la madai kinzani.
Kampuni hiyo iliingia mikataba na benki hizo kwa nyakati tofauti katika ya mwaka Septemba 28, 2020 na Oktoba 5, 2021, ambapo benki hizo ziliiwekea udhamini wa mkopo kutoka kwa mkopeshaji wa nje ya Nchi, kwa ajili ya kulipa madeni yake mengine na kuendesha shughuli zake.
Mikataba hiyo iliiwezesha kampuni hiyo kupata mkopo wa Dola za Marekani 7,013,000 ( zaidi ya Sh18.43 bilioni) kitoka kampuni ya Lamar Commodity Trading DMCC (Lamar) kutoka Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu kupitia wakala wake kampuni ya Numora Trading PTE Limited (Numora)
Kwa mujibu wa mkataba wa mkopo huo, benki hizo zilipaswa kwanza kuwasilisha kwa kampuni hiyo hati ya muamana yaani barua ya Kibenki ya udhamini wa mkopo huo (Standby Letter of Credit/Letter of Credit – SBLC/LC) kama sharti la mkopo huo, ambalo benki hizo zililitekeleza.
Ili kupata SBLC/LC hiyo, kampuni hiyo ya ZAS mbayo ilikuwa mteja wa benki hizo tangu mwaka 2014, pia iliweka hati za mali ze.mbalimbali zinazohamishika na zisizohamishika zilizoko.katika maeneo mbalimbali nchini, kama dhamana.
Hata hivyo baada ya muda wa kurejesha mkopo huo kufika kampuni hiyo ya ZAS ilishindwa kuureresha na hivyo benki hizo kama.mdhamimi zikawajibika kuilipa mkopo huo na zenyewe zikaidai kampuni hiyo.
Badala ya kulipa mkopo huo, kampuni hiyo ilikimbilia mahakama.amnako ilifungua kesi kupinga kudaiwa na benki hizo kwa madai kuwa mkopo huo ilioupokea kutoka kwa mkopeshaji huyo wa nje, hakuwa na dhamana.
Katika kesi hiyo ya kibiashara namba 103 ya mwaka 2022, kampuni hiyo ya ZAS ilidai kuwa mikataba iliyosainiwa na pande hizo mbili kuwezesha upatikanaji wa mkopo huo ni batili, ikidai kuwa benki hizo zilikiuka masharti kwa kushindwa kuitekeleza, kwa kuwa hazikutoa SBLC/LC hiyo.
Kwa hiyo kampuni hiyo ilidai kuwa mkopo huo ilioupokea kutoka kampuni ya Lamar/Numora hakuwa na dhamana kutoka kwa benki hizo, huku ikizituhumu benki hizo kufanya udanganyifu na kuhusiana na upatikanaji mkopo huo na kusababisha kuilipa zaidi ya Dola za Marekani 300,000 isivyo halali.
Hivyo iliiomba pamoja na mambo mengine mahakama hiyo iamuru kuwa benki hizo zilikiuka masharti ya mikataba hiyo na iamuru kwamba mali ilizoziweka.kama.dhamana ya kuwezesha kupata mkopo huo wa nje zilizosajiliwa na benki hizo zilisajiliwa isivyo halali na ziachiliwa na kuirejeshea.
Benki hizo katika majibu yake zilipinga madai hayo ya kampuni hiyo huku nazo zikifungua shauri la madai kinzani dhidi ya kampuni hiyo ya ZAS na wakurugenzi wa kampuni hiyo waliotoa udhamini binafsi na kinga kwa ajili ya SBLC/LC hiyo.
Wadhamini hao ambao ni wakurugenzi wa kampuni hiyo ni Amit Babubhai Ladwa, Muzdalifat Mohamed Ali, Jamal Ali Muslim pamoja na kampuni za Masasi Construction Company Limited na Bahati Apartment.
Katika madai yake hayo benki hizo zilidai kuwa zilitekeleza masharti ya mikataba hiyo kwa kuwa zilitoa SBLC/LC iliyoiwezeaha kampuni hiyo kupata mkopo huo kutoka kwa Lamar/Numero.
Zilidai kuwa kampuni hiyo ndio iliyokiuka masharti ya mkabata kwani jaikuweza kurejesha mkopo huo kwa mkopeshaji na zenyewe ndio zikawajibika kuulipa.
Wakati wa usikilizwaji wa kesi hiyo iliyosikilizwa na Jaji Butamo Phillip, kampuni ya ZAS iliyowakilishwa na Wakili Frank Mwalongo, ilimuita shahidi mmoja na kuwasilisha jumla ya vielelezo 18.
Benki za Equity ambazo ziliwakikishwa na Wakili Timon Vitalis ziliwaita mashahidi wanne huku zikiwasilisha kupitia mashahidi hao jumla ya vielelezo 95.
Mahakama baada ya kusikiliza na kupitia ushahidi wa pande zote, vielelezo vilivyowasilishwa pamoja na hoja za mwisho za mawakili wa pande zote katika uamuzi wake ilioutoa juzi, Jumanne Alhamisi Julai 23, 2024, imetupilia mbali shauri la msingi lililofunguliwa na ZAS.
Mahakama hiyo imefikia uamuzi huo baada ya kujiridhisha kuwa madai na hoja za kampuni hiyo hazina mashiko kwani ilishindwa kuyatbibitisha madai yake.
Badala yake imekubaliana na madai ya Benki hizo na hoja za Wakili wake, Vitalis, ilisema kuwa zimeweza kuthibitisha madai yake kwa kiwango kinachohitajika kisheria.
Pamoja na mambo mengine msingi wa kesi ya upande wa mdai (ZAS) katika kesi hii ilikuwa ni kwamba mkopo ilioupata kutoka kwa Lamar/Numora si tu haukuwa na dhamana ya SBLC/LC kutoka kwa Benki ya Equity Kenya (EBK) Bali pia haukuwa na dhamana hiyo kutoka mahali popote.
Katika hoja zake Wakili wa ZAs, Mwalongo aliieleza Mahakama kuwa swali kwamba iliwezekwanaje mkopeshaji Lamar/Numora akatoa mkopo huo bila ya dhamana ya SBLC/LC kama mkataba wa mkopo huo unavyoeleza, haikuwa hoja inayohusika katika kesi hiyo.
Wakili Mwalongo alidai kuwa pande husika katika mkopo huo ndizo zinajua sababu hiyo na kwamba hivyo mahakama haikupaswa kujishugulisha nayo.
Hoja hiyo ilipingwa vikali na Wakili wa EBT na EBK, Vitalis ambaye aliirejesha Mahakama katika kielelezo cha 64 cha upande wa utetezi (benki hizo) yaani barua ya dhamana ya EBK (LC) ni sharti muhimu lililopaswa kutekelezwa kwanza ndipo mkopeshaji atoe mkopo huo.
Lakini Jaji Phillip amesema kuwa hakubaliani na wakili Mwalongo, kuwa mkopo huo uliotolewa bila SBLC/LC, kinyume cha kielelezo cha Sita cha upande wa mdai (ZAS), mkataba baina yake na mkopeshaji Lamar/Numora, kuwa hoja hiyo si sehemu ya kesi hiyo.
Jaji Phillip amesema hata shahidi wa kwanza wa mdai, ZAS alisema kuwa hoja hiyo ni inahusika.katika kesi hiyo Ili kuamua mgogoro wa utolewaji wa hiyo SBLC/CL.
“ZAS inadai kuwa kuna ukiukwaji wa makubaliano ya SBLC/LC na wakati huohuo imedai kuwa ilipokea mkopo huo kiasi kikichooneshwa kwenye SBLC/LC bila kuwepo kwa SBLC/LC hiyo”, amesema Jaji Phillip na kuongeza:
“Hivyo ilikuwa muhimu ZAS kuelezea iliwezaje kupata mkopo uliopaswa kuwa na dhamana ya SBLC/LC, bila kuwepo hiyo SBLC/LC”.
Jaji Phillip amesema kuwa hawezi kusisitiza umuhimu wa maelezo ya mkopo unaodajwa kutolewa na Numora bila dhamana katika kesi hiyo.
“Itoshe tu kusema kwamba kwa kuwa EBT na EBK walidai kuwa LC ilitolewa na kuwezesha utolewaji wa mkopo kwa ZAS kutoka Lamar/Numora, ZAS ina dhima ya kuthibitisha madai yake kuwa mkopo huo haukuwa na dhamana ya SBLC/LC iliyotolewa na EBK”, amesema Jaji Phillip.
Amesisitiza kuwa madai ya wakili Mwalongo kuwa mkopo huo haukuwa na dhamana hayana msingi na kwamba ushahidi uliotolewa unathibitisha kwamba mkpo huo ulitolewa kwa ZAS baada ya kutolewa kwa LC.
Pia amesema kuwa ushahidi unaonesha kwamba EBK ilipaswa kulipa kiasi cha mkopo huo chini ya masharti ya LC na kwamba ZAS haikuweza kutoa ushahidi kuthibitisha kuwa iliilipa EBK kiasi cha mkopo huo ambao EBK iliulipa (kwa Lamar/Numora).
Hivyo Jaji Phillip baada ya kuchambua na kujadili ushahidi wa pande zote, vielelezo na hoja za mawakili, amehutimisha kuwa kuwa SBLC/LC na EBK kwa ajili ya mkopo huo uliotolewa kwa ZAS kutoka Lamar/ Numora.
Pia amesema kuwa mikataba ya mikopo hiyo baina ya ZAS na EBT na EBK Septemba 28, 2020 na Oktoba 5, 2021 si batili kwani ilitekelezwa na kwamba ZAS ilikiuka mikamata hiyo kwa kushindwa kurejesha mkopo huo ndani ya muda uliokubaliwa.
“Kwa nyongeza ushahidi uliotolewa na EBT na EBK ulithibitisha kwa kiwango kinachotakiwa kisheria kwamba ZAS inadaiwa na EBT na EBK”, amesema Jaji Phillip.
Pia amesema kuwa ushahidi huo uliotolewa umethibitisha kwamba wadaiwa wa pili mpaka wa sita katika madai kinzani (ya EBT na EBK) wanawajibika kulipa mkopo uliotolewa kwa ZAS katika nafasi yao ya udhamini.
“Kutokana na hayo (yaliyoelezwa) ni uamuzi wa mahakama hii kwamba ZAS imeshindwa kuthibitisha madai yake dhidi ya EBT na EBK, kwa kiwango kinachotakiwa kisheria, wakati EBT na EBK zimeweza kuthibitisha madai yake dhidi ya wadaiwa katika madai kinzani kwa kiwango kinachotakiwa kisheria”, amesema jaji na kuhitimisha:
“Hivyo ninafuta kesi ya msingi kwa gharama (mdai, ZAS kulipa gharama gharama za kesi) na ninatoa hukumu dhidi ya wadaiwa katika madai kinzani (ZAS na wadhamini wake) kama ifuatavyo”, amesema Jaji Phillip na kutoa amri mbalimbali.
Kesi hii ni moja kati ya kesi kadhaa zilizofunguliwa na kampuni mbalimbali zinazodaiwa kukopeshwa au kudhaminiwa na benki hizo kupata mikopo kutoka kwa wakopeshaji wa nje lakini zikagoma kulipa na kisha kuzishtaki benki hizo baada ya kuzidai, zikipinga kudaiwa.
Kampuni hizo ambazo zote zinawakilishwa na wakili mmoja, Mwalongo, ziko katika maeneo tofautitofauti na zilikopa kwa nyakati tofauti lakini msingi wa mgogoro wao dhidi ya benki hizo katika ulipaji wa mikopo hiyo unafanana na karibu zote zinapinga kudhaminiwa na benki hizo
Mwisho wa kuunukuu mtandao huo Soma hapa chini HUKUMU NZIMA YA KESI HIYO CHECHEFU