Alfajir ya kuamkia Leo tarehe 14/01/2025 imechechezwa michezo sita katika ligi ya mpira wa kikapu Marekani (NBA) ambapo michezo minne imemalizika na mingine miwili ikiwa inaendelea.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0001.jpg)
Michezo iliyo malizika.
Washington wizards dhidi ya Minnesota Timberwolves ambapo mchezo huo umechezwa katika uwanja wa Capital One Arena na kumalizika kwa Minnesota Timberwolves kuibuka na ushindi wa vikapu 120 dhidi ya vikapu 106.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0007-1024x576.jpg)
New York Knicks dhidi ya Detroit Pistons ambapo mchezo huu ulimalizika kwa Detroit Pistons kushindwa kwa vikapu 124 dhidi ya vikapu 119, mchezo huo uliopigwa nyumbani kwa New York Knicks katika dimba la Madison Square garden na kuhudhuriwa na mashabiki 19,812.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0006.jpg)
Toronto raptors dhidi ya Golden State warriors ambapo Toronto raptors wameigalagaza Golden State warriors kwa vikapu 104 dhidi ya vikapu 101 katika mchezo huo uliopigwaa kwenye dimba la Scotiabank Arena huku mashabiki walio hudhuria ni 19,165.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0005-1024x682.jpg)
Huston Rockets dhidi ya Memphis Grizzlies uliochezwa katika dimba la Toyota Center ambapo Huston Rockets wameibuka na ushindi wa vikapu 120 dhidi ya vikapu 118 vya Grizzlies huku mashabiki walio hudhuria wakiwa ni 18,055.Michezo inayoendelea.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0004-1024x682.jpg)
LA Clippers dhidi ya Miami Heat mchezo huu unapigwa kwenye uwanja wa Intuit Dome ikiwa ni mapumziko Miami akiongoza kwa vikapu 48 dhidi ya vikapu 43 vya Clippers.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0003-1024x682.jpg)
LA Lakers dhidi ya San Antonio Spurs ambapo mchezo huo unapigwa kwenye uwanja wa Crypto. Com Arena ikiwa ni mapumziko Lakers wakiwa wanaongoza kwa vikapu 62 dhidi ya vikapu 53 vya San Antonio Spurs.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0002-1024x683.jpg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/01/IMG-20250114-WA0000.jpg)