- Ni katika kesi ndogo ndani ya kesi kubwa baina ya Continental Reliable Clearance ‘CRC’ dhidi ya Benki ya Equity waliofungua kupinga kurejesha mkopo wa shilingi bilioni 26 waliokopeshwa na benki hiyo chini ya wakili Mwalongo
Na Mwandishi wetu,
Mahakama Kuu Division ya Biashara imetoa hukumu ndogo ya nyaraka za miamala ya Benki zilizowasilishwa na Shahidi ya wa pili Elexender Gombanila za kutoingizwa katika vielelezo vya ushahidi katika kesi ya Equity na CRC .
Kampuni ya CRC inayotetewa na Wakili Frank Mwalongo katika Mahakama Kuu Division ya Biashara huku upande walalamikiwa wa Equity wakitetewa na Wakili Emmanuel Saghan na Mpaya Kamala
Hukumu hiyo imetolewa na Jaji Profesa Ubena Agatho baada ya upande wa mawakili wa walalamikiwa kuwasilisha hoja ya nyaraka za utoaji Mikopo kutozingatia matakwa ya kisheria kutumika katika vielelezo vya ushahidi katika kesi hiyo.
Wakili Emmanuel Saghan na Mpaya Kamala walipinga kupokea sehemu ya vielelezo vilivyotakiwa kutumika katika kesi hiyo baina ya CRC na Benki ya Equity
Katika kesi hiyo shahidi wa pili upande walalamikaji Elexender Gombanila amewasilisha nyaraka mbalimbali ikiwa ndio ushahidi katika kesi hiyo ya mkopo Chechefu ya shauri la biashara Namba 16 la Mwaka 2023 kati ya kampuni ya CONTINENTAL RELIABLE CLEARING (T) LIMITED ambaye ni mdai katika kesi hiyo Dhidi ya EQUITY BANK TANZANIA LIMITED na Equity BANK KENYA LIMITED ambao ni wadaiwa. Kesi hiyo inayohusiana na mkopo chechefu inasikilizwa mbele ya Mheshimiwa Jaji Professa Ubena Agatho wa Mahakama Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara.
Katika kesi hiyo ya kampuni ya CONTINENTAL RELIABLE CLEARING (T) LIMITED iliyofunguliwa Mwaka 2023 mdai anaiomba mahakama pamoja na mambo mengine kutoa amri dhidi ya wadaiwa ya kuwa wadaiwa ambao ni taasisi za kibenki wamevunja mikataba ya mikopo na kuvunja wajibu wa benki dhidi ya mdai kama mteja. Pili, Mahakama itamke ya kuwa mdai amelipa mikopo yake yote na hadaiwi. Tatu, Mahakama itamke ya kuwa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni kumi (10,139,664.95) ambazo wadaiwa kwa pamoja wamemtaka mdai alipe kama kiasi cha mkopo ambacho hakijalipwa sio halali na hakijawahi kuwepo. Nne, Mahakama itamke ya kuwa mikopo inayodaiwa kutolewa tarehe 29/05/2018, 3/11/2021 na tarehe 19/02/2022 ni batili. Tano, Mahakama itamke ya kuwa mikopo iliyotolewa tarehe 1-02-2019 na tarehe 17-09-2020 haijawahi kutekelezwa na mdaiwa namba mbili ambaye ni Equity Bank Kenya isipokuwa kwa kiasi Fulani ilitekelezwa na mdaiwa namba moja ambaye ni Equity Bank Tanzania.
Sita, Mahakama itamke ya kuwa mikataba ya dhamana zote zisizohamishika zilizowekwa kwa wadaiwa kudhamini mikopo na mdai ni batili. Saba, Mahakama itoe tamko ya kuziondoa dhamana hizo kwenye mikopo na kuzikabidhi kwa mdai. Nane, Mahakama itamke ya kuwa tamko la kutaka wadaiwa walipwe fedha za mkopo na mdai ni batili. Tisa, Mahakama itamke ya kuwa Equity Bank Kenya ambaye ni mdaiwa namba mbili hana leseni ya kuendesha shughuli au biashara ya kibenki au biashara yeyote Tanzania na hivyo amefanya biashara kinyume cha sheria tofouti na matakwa ya kanuni na miongozo inayohusiana na biashara za kibenki nchini Tanzania. Kumi, Mahakama itamke ya kwamba mdaiwa namba mbili amabye ni Equity Bank Kenya hajawahi kutoa au kumpatia mkopo mdai. Kumi na moja, fidia, gharama za kesi na nafuu nyinginezo ambazo mahakama itaona sahihi kuzitoa kwa mdai dhidi ya wadaiwa.
Chimbuko la kesi hii inadaiwa kuwa kwa mujibu wa hati ya madai iliyowasilishwa mahakamani hapo, kati ya Mwaka 2013 mpaka 2017 mdai alikuwa ni mteja wa mdaiwa namba moja, Equity Bank Tanzania. Kwa kipindi chote hicho, mdaiwa alipatiwa mikopo mbalimbali ambayo inafikia minane kwa ajili ya kuendesha biashara zake miongoni mwazo ni biashara ya usafirishaji wa mizigo na mafuta kwa kutumia magari. Ilipofika kuanzia mwaka May 2018 ndipo mdaiwa Equity Bank Kenya alipoanza kuingia kwa kushirikiana na mdaiwa namba moja kwa pamoja kumkopesha mdai.
Kiini cha mgogoro haswa ni mikopo inayodaiwa kutolewa na wadaiwa wote wawili Kwenda kwa mdai iliyosainiwa 29/05/2018, 3/11/2021 na 19/01/2022 kati ya mdai na wadaiwa wote wawili ambapo kwa mujibu wa wadaiwa wanadai kuwa mdai hajalipa kiasi cha dola za kimarekani zaidi ya milioni kumi na hivyo kumtaka alipe pesa hivyo kama alivyokopa kulingana na mikataba ya mikopo. Kwa upande wa mdai anapinga madai ya kulipa pesa hizo kwa sababu ya kuwa ingawa wakopeshaji wametajwa wote wawili kwenye mikopo hiyo, lakini mdaiwa hajawahi kuingiziwa fedha zozote na Equity Bank Kenya wala kulipa pesa zozote kwa Equity Bank Kenya. Na kuhusu fedha alizokopeshwa na Equity Bank Tanzania mdai anasema kuwa aliendelea kuzilipa na ulipaji huo ulithibitishwa kila mara na mdaiwa wa kwanza.
Kwa upande way a majibu ya utetezi yaliyowasilishwa mahakamani kwa pamoja na wadaiwa wote wawili, wanapinga hoja au madai yote yaliwasilishwa mahakamani na mdai na kuiomba mahakama iyatupilie mbali kwa kuwa mdaiwa alikopa kihalali kutoka kwa wadaiwa wote wawili na kwa nyakati tofauti kati ya tarehe 27/05/2020, 19/01/2023, 26/01/2023 na 26/02/2023 mdaiwa kupitia mawasiliano kwa njia ya barua pepe na barua nyingine zilizoandikwa Kwenda kwa wadaiwa alithibitisha kutolewa kwa fedha hizo za mikopo na hivyo hawezi kuitaka mahakama kubatilisha mikataba ya mikopo hiyo baada ya kushindwa kuilipa au kurejesha.
Kesi hiyo leo ilipokuja kuendelea na usikilizwaji, upande wa mdai uliendelea kutoa Ushahidi wake kwa shahidi namba mbili upande wa mdai ambaye Elexender Gombanila
la Upande wa mdai uliwakilishwa na Wakili Msomi Frank Mwalongo ambaye alikuwa wakili kiongozi na upande upande wa wadaiwa uliwakilishwa na Wakili Emmanuel Kagali akimuwakilisha Equity Bank Tanzania Ltd na Wakili Mpaya Kamala akimuwakilisha Equity Bank Kenya Ltd.
Baada ya kuapishwa na Mahakama, shahidi namba mbili wa upande wa mdai aliweza kuwasilisha vielelezo vya Ushahidi ambazo ni nakala 8 za miamala ya Equity Bank (Bank Statements) za kati ya 2013 na 2017 pamoja na barua pepe ambazo zilipokelewa na mahakama bila pingamizi lolote kutoka upande wa utetezi.
Tatizo lilianzia pale ambapo shahidi alitaka kuwasilisha nakala za miamala ya kifedha nne (bank statements) za kati ya 2018 hadi 2022 ambapo zilikumbana na mapingamizi ya kisheria kutoka kwa mawakili wa utetezi. Mapingamizi hayo yalitolewa kupinga kupokelewa kwa nakala hizo za miamala ya kibenki ni kuwa Kiapo cha uthibitisho wa usahihi wa nakala hizo kuwa zimetoka Equity Banks zipo kinyume na sheria ya Ushahidi Sura ya 6 hasa kifungu namba 76, 77 na 78. Vilevile shahidi huyo sio afisa wa benki au Partner wa benki hivyo hana uhalali wa kuzitoa nyaraka hizo.
Wakili Saghan alieleza Mahakama kuwa nyaraka hizo hazijawahi kuwasilishwa au kuongelewa wakati kesi hiyo inafunguliwa kinyume na sheria inayoongoza taratibu za uendeshaji wa kesi za madai (Civil Procedure Code).
Mahakama katika uamuzi wake ilikubaliana kutopokea vielelezo yaliyowasilishwa na mawakili wa upande wa utetezi kuwa hayana mashiko kisheria na hivyo kukataa kupokea nyaraka hizo.
Sababu za kukubaliana na hoja za mawakili wa utetezi juu ya mapingamizi yao ya kisheria ni kuwa kiapo cha shahidi juu ya uthibitisho wa usahihi na uhalali wa taarifa za miamala (bank statements) kinakinzana na matakwa ya kifungu cha 76,77 na 78 ya sheria ya Ushahidi (Evidence Act) Sura 6) kwa kuwa nyaraka hizo hazina sahihi wala muhuri wa benki kwa uthibitisho kuwa zimetoka benki.
Pia shahidi huyo sio afisa au partner wa benki kwa kuwa hakuna sehemu yeyote amethibitisha au kusema kuwa anatokea benki kinyume na sheria ya Ushahidi. Na mwisho, nyaraka hizo hazikuwa sehemu ya nyaraka zilizowasilishwa mahakamani wakati wa kufunguliwa kwa kesi hiyo kinyume na matakwa ya sheria za mwenendo wa mashauri ya madai.
Baada ya kusoma uamuzi huo mdogo na kukataliwa kupokelewa kwa nyaraka hizo.
Baada ya hukumu hiyo sehemu mdogo ya ushahidi kutoingizwa kuwa vielelezo vya ushahidi katika kesi imeahirishwa mpaka Julai 2 Mwaka huu katika Mahakama Kuu ya Biashara