– Wanufaika wa mikopo hiyo, wapambe wao wahaha kujikwamua
– Orodha ya makampuni ya wanaochezesha michezo chechefu yazidi kuongezeka
– Wengine wakabidhi dhamana feki benki, wengine wauza dhamana huku nyaraka zikiwa benki
– Ripoti CAG yaanika madudu ya benki za kimkakati za TCB, AZANIA na TADB
– Yaonyesha namna mabilioni ya wananchi yanavyotafunwa bila huruma
– Jamvilahabari kuendelea kuupasha umma kila kitu licha ya vitisho
Na. Omary Kihampa
Hali imezidi kuwa tete miongoni mwa wafanyabiashara waliochota mabilioni ya pesa katika mabenki mbalimbali nchini nan je ya nchi na kisha kukataa kulipa kwa njia mbalimbali ikiwemo kukimbilia mahakamani ambako kwa namna za kutatanisha baadhi yao wameibuka washindi kwa mahakama kuu divisheni ya biashara kuwapa haki ya kutokulipa mikopo hiyo na sasa wafanyabiashara hao wanahaha .
Kitendo cha mahakama ya rufaa kutengua hukumu iliyowapa ushindi kampuni ya State Oil dhidi ya benki ya Equity Tanzania na Equity Kenya na kuelekeza shauri hilo lianze kusikilizwa upya katika mahakama ya biashara kimefanya wanufaika wa mikopo hiyo, wapambe wao kuhaha kujikwamua wakihofia mwenendo wa mashauri yao yatakavyokuwa ikiwa haki itaachwa itendene
Hilo linajiri wakati orodha ya makampuni ya wanaochezesha michezo chechefu yazidi kuongezeka kuongezeka na mashauri mahakamani kuendelea kusikilizwa ikiwemo shauri baina ya Continental Reliable Clearing ambaye kama ilivyo kwa state oil, TSN, KOM na wengine wanatetewa na wakili frank mwalongo wa kampuni ya uwakili ya Apex attorneys wakiitaka mahakama iwazuie kuwalipa benki ya Equity katika mkopo wa zaidi ya shilingi bilioni 25 za kitanzania waliouchukua kwa nyakati tofauti katika benki hiyo
Taarifa za uhakika ambazo gazeti hili imezipata zinaonyesha kuwa pamoja na makampuni hayo kuchezesha mahakamani wakitumia watendaji wa mahakama wasio waaminifu, lakini pia makampuni hayo yamekuwa yakikabidhi dhamana feki benki na wengine wauza dhamana huku nyaraka zikiwa benki
Katika ripoti ya mdhibiti na mkakuzi mkuu wa serikali nchini aliyoitoa mwezi machi mwaka huu, ameanika madudu ya benki za kimkakati za za serikali za TCB, AZANIA na TADB yanayoonyesha namna mabilioni ya wananchi yanavyotafunwa bila huruma
Hivi karibuni gazeti hili litandelea kuupasha umma kila kitu bila kificho kuhusiana na kinachoendelea katika mikopo hiyo chechefu na washirika wake.