- Ni ya uenyekiti wa CHADEMA
- Aliingia madarakani akimpokea Bob Makani mwaka 2004
- watoto waliozaliwa wakati anaingia madarakani leo chuo kikuu wengine wana watoto
- amefanya kazi na makamu wenyeviti watano tangu aingie madarakani
- wamo marehemu Kaboru, Marehemu Wangwe, Mzee Said Arfi, Prof. Abdullah Safari na Tundu Lissu wa sasa.
- inaaminika anajiandaa kugombea tena mwaka huu ili azidi kuvunja rekodi ya kukaa madarakani miaka 25
- mipango ya yeye kupita bila kupingwa uenyekiti imewiva, wanaoutamani uenyekiti wake kukiona cha moto
Na. Mwandishi wetu,
Imetimia miaka 20 kamili tangu kuingia madarakani kwa mwemyekiti wa chama cha Demokrasia na maendeleo CHADEMA Freeman Aikael Mbowe maarufu kama Kamanda wa Anga ama Kaka Mbowe kama wanavyomuita wakazi wa Hai mkoani Kilimanjaro
Mbowe ambaye mwaka 2000 alishinda ubunge wa jimbo la hai kwa mara ya kwanza baada ya kushindwa mwaka 1995 aligombea Urais wa Tanzania mwaka 2005 na kuwa miongoni mwa wagombea watano waliomfuatia mshindi wa uchaguzi huo Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete aliyewagaragaza sambamba na Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF, Augistine Mrema wa TLP, Freeman Mbowe wa CHADEMA na wengineo
Ni katika uchaguzi huo ndipo Mbowe aliibuka na staili mpya ya kukitangaza chama hicho kwa kusafiri akitumia helkopta huku akivaa mavazi ya aina yake maarufu kama kombati za CHADEMA
Katika uchaguzi huo wa mwaka 2005, mwaka mmoja tangu akabidhiwe chama na mtangulizi wake marehemu Bob (Ramadhani) Nyanga Makani, alifanikiwa kukisaidia chama chake kupata wabunge watano wa kuchaguliwa na wabunge sita wa viti maalum na kufanya chama hicho kupata jumla ya wabunge 11
Miongoni mwa wabunge waliopatikana katika uchaguzi huo ni pamoja na Zitto Zuberi Kabwe (Kigoma Kaskazini), Marehemu Chacha Zakayo Wangwe (Tarime), Marehemu Philmon Ndesamburo (Moshi Mjini), Dkt. Wilbrod Peter Slaa (Karatu) na Said Amour Arfi (Mpanda kati)
Wabunge wa viti maalu ni Maulida Komu, Halima James mdee, Grace Sindato Kihwelu, Suzan Lyimo na Muhonga Said Ruhwanya
Wakati Mbowe anakuwa mwenyekiti wa CHADEMA Taifa kwa mara ya kwanza, Dokta Walid Amani kaburu alichaguliwa kuwa makamu mwenyekiti wake akiwakilisha Tanzania bara
Miaka michache baada ya mbowe kuwa mwenyekiti akisaidiwa na Dkt. Kaburu, taarifa zinasema kuwa maelewano kati yao hayakuwa mazuri kiasi cha kaburu kuamua kuachia ngazi na kujiunga na chama cha Mapinduzi CCM
Kuondoka kwa Kaburu na kuacha nafasi wazi ya umakamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania bara, kulipelekea baraza kuu la chama hicho kuitisha uchaguzi wa kuziba nafasi hiyo ambapo aliyekuwa mbunge wa Tarime mjini wakati huo Marehemu Chacha Zakayo Wangwe alishinda uchaguzi na kuwa makamu mwenyekiti wa chama hicho Tanzania bara akichukua nafasi iliyokimbiwa na kaburu
Kumbukumbu zinaonyesha kuwa haikumchukua muda mrefu Wangwe kushindana tabia na mwenyekiti wake Mbowe na makamu huyo kupingana hadharani na kupinga namna mwenyekiti huyo alivyokuwa anakiendesha chama hicho na kuibua tuhuma kadhaa kumuhusu yeye tuhuma ambazo hadi hivi sasa hazijapata majibu
Taarifa zinaonyesha zaidi kuwa kitendo cha marehemu Wangwe kumpinga Mbowe hadharani kilimpelekea kusukiwa mpango wa kusimamishwa uenyekiti na wiki chache baadae Wangwe akafariki kwa ajali ya gari iliyotokea Pandambili mkoani Dodoma
Ni baada ya kufariki kwa chacha wangwe ndipo Said Amour Arfi akachukua nafasi ya umakamu mwenyekiti kuziba pengo hilo hadi naye alipokuja kurithiwa na Prof. Abdullah Safari
Prof. Safari akiwa makamu mwenyekiti wa nne katika utawala wa mwenyekiti Mbowe alimuachia kitu makamu wa sasa Tundu Antipas Lissu
Hesabu za kawaida za gazeti hili zinaonyesha kuwa kuwa kiongozi wa chama cha siasa kwa miaka 20 mfululizo ni tukio la aina yake kama sio la kihistoria ulizingatia kuwa watoto waliozaliwa mwaka 2004 wakati Mbowe anaingia madarakani tayari wameshaanza darasa la kwanza na kufika chuo kikuu na wale ambao hawakuendelea na masomo hivi sasa wameshaoa na kuoleea na wengine tayari wamezaa
“Kwa kifupi mwenyekiti wetu ni miongoni mwa wenyeviti wakongwe hapa nchini, na tunajivunia ukongwe wake kwa kweli, miaka 20 madarakani si haba”. Anasema mmoja wa wenyeviti wa wilaya wa chama hicho
” hebu fikiria ameingia madarakani Rais akiwa Marehemu Mkapa, akakaa miaka 10 yote ya Kikwete, akaja na Magufuli na sasa yupo na Samia na bado mwenyekiti wetu anadunda tu na anaweza Samia kuondoka Ikulu akaja mwengine na yeye akaendelea, nasisi hatuna shida nae akae hata miaka 50, mpana aseme mwenyewe nimechoka”. Ameongeza
Itaendelea matoleo yajayo