MANYARA – Na Mwandishi wetu
Waumini wa Dini ya Kiislamu wa Kata za Galapo na Kashi kwa pamoja wamejumuika kumuombea Dua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan na Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Daniel Sillo.
Wazikungumza leo Aprili 07, 2024 katika Kata ya Kashi Kitongoji cha Migungani Wilayani Babati Mkoani Manyara wakati wa Harambee ya Ujenzi wa Madrasa baada ya kuomba Dua walimpongeza na kumshukuru Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kumteua Mhe. Sillo kuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi ambapo wamemuomba afanye kila ambalo ni jema na matarajio ya Mhe. Rais
“Tumekuwa na desturi ya kuwaoombea Viongozi wetu na leo tumewiwa kukuombea Dua kwa kazi nzuri unayoifanya ya kutuwakilisha na matokeo bora ya utendaji kazi wako Mhe. Rais amekuamini na kukuteua katika nafasi hiyo ambayo utakuwa unatumika Kitaifa” Walisema.
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Daniel Sillo alitumia nafasi hiyo kumshukuru na kumpongeza Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa nia njema aliyoonesha ya kuwaoongoza Watanzania pia aliwataka waumini hao wasichoke kumuombea awe na afya njema ili aendelee kutuletea Maendeleo.
Aidha, Mhe. Sillo aliwashukuru Waumini hao kwa Dua hiyo njema pamoja na wananchi wote wa Jimbo la Babati Vijijini kwa umoja na mshikamano wao na kuwaomba ushirikiano zaidi katika kusukuma gurudumu la Maendeleo kwani maendeleo hayana Chama, Dini wala Kabila.