DKT. BITEKO AFICHUA ORODHA YA HATARI MATENDO YA UHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA TANESCO
Na. Mwandishi wetu
Naibu Waziri mkuu na waziri wa Nishati nchini Dkt. Doto Mashaka Biteko, ameelekeza kuondolewa kazini haraka kwa wtumishi wote wa Tanesco wanaojihusisha na mtandao wa uhujumu wa miundombinu ya shirika hilo ikiwemo wizi wa mafuta ya transfoma, wizi wa Nyaya, wizi wa transfoma na vifaa vinginevyo muhimu
Dkt. Biteko amesikitishwa na kukithiri kwa matendo ya uhujumu wa miundombinu ya umeme nhini na kubainisha kuwa yapo matendo yanayotendwa na wahalifu wa kawaida lakini yapo mengine ambayo waharifu hao hushirikiana na watumishi wa Tanesco
Akizungumza katika kikao kazi kati yake na watendaji wa Tanesco na kampuni tanzu zilizo chini ya shirika hilo Biteko amesisitiza kuwa ni wajibu wa Tanesco kuhakikisha inatoa huduma kwa wananchi kwa viwangi vya juu kuondoa mtazamo hasi walio nao wananchi juu ya shirika hilo na kuonyesha kukerwa kwake na kufumbiwa macho watumishi waliokamatwa na vidhibiti mikononi mwao wakishiriki uhujumu wa miundombinu ya shirika hilo
‘’Hujuma ya miundombinu hii ni kweli ipo inayosababishwa na watu wasio waaminifu, lakini ipo inayosababishwa na Cartel (mtandao) ya watu wetu huko chini na watu wasiokua waaminifu, sasa wizi wenyewe unaofanyika ni wa aina saba wa kwanza wizi wa vifaa vyenye asili ya shaba, wa pili wizi wa vyuma vya nguzo kwenye nguzo za kusafirisha umeme mkubwa, wizi wa mafuta ya transfoma, wizi wa vifaa mbalimbali vya kujenga miradi, ujenzi wa laini haramu..tunao mtu wa Tanesco ambao yeye mwenyewe kajipa kazi, kaiba vifaa, kalipwa yeye hela, kaenda kujenga laini ambayo hakuna mtu anayeijua, kaijenga laini mpaka mwisho kilometa moja na nusu na hela kalipwa. Hela hiyo haikuingia Tanesco. Ni kweli mwananchi amepata umeme lakini hadi mita kwenye rejesta haipo…halafu kuna la Rushwa pamoja na la vishoka’’. Amesema Dkt. Biteko
NUKUU ZA DKT. BITEKO AFICHUA ORODHA YA HATARI MATENDO YA UHUJUMU WA MIUNDOMBINU YA TANESCO
1. ‘’Tarehe 13 mwezi wa pili mwaka 2024, BAGAMOYO alikamatwa mtu mmoja pale akiwa na Lita 80 za mafuta ya Transfoma, kesi imefunguliwa, maana yake ile Transfoma imekufa mafuta yamesha chukuliwa’’
2. ‘’Mwezi wa tatu tarehe tatu ubungo maziwa Dar es Salaam, amekamatwa mtu jina ninaye hapa akiwa na lita 400 za mafuta ya Transfoma kesi inaendelea na upelelezi unaendelea’’
3. ‘’tarehe moja mwezi tatu Keko Dar es salaam, mwananchi mmoja amekamatwa na kilo 50 za Nyaya ya shaba zenye thamani ya shilingi laki saba na Hamsini, na hawa kuna kiwanda kimoja kila tukio la waya unaona walikuwa wanaenda kushusha kwenye kiwanda hicho, kwa sababu tuko katika upelelezi sitaki kuki disclose. Hawa nao kesi inaendelea’’
4. ‘’baadae Kilo 361 za Nyaya zenyewe zimekamatwa, wapi keko Dar es salaam , keko hiyo hiyo kilo nyingine 1105 zimekamatwa na zilikuwa zinapelekwa kwenye kiwand kile kile zinaenda kuuzwa, zenye thamani ya shilingi milioni 16,575,000/=’’.
5. ‘’Mwezi wa tatu Dar es salaam Keko, kilo 57 za shaba, Bunju Dar es salaam na kwenyewe amekamatwa mtu mmoja lakini ana material zenye thamani ya shilingi milioni 200 mali ya Tanesco kesi inaendelea na upelelezi unaendelea’’.
6. ‘’Tarehe 17 mwezi wa tatu, sisi tupo kwenye maombolezo wenyewe wanaiba, Kigamboni na huyu ni mfanyakazi wetu wa muda maalum anaitwa Hussein Yusuph Rashidi wa kigamboni kaiba copper wire roller nzima na transfoma iliyokuwa kwenye matengenezo ameenda kuuza apate hela. Kesi ipo Mahakamani’’.
7. ‘’Ubungo maziwa tena huyu sio mfanyakazi wa Tanesco , wameiba transfoma tatu kesi inaendelea’’
8. ‘’ Tarehe 21 mwezi wa tatu, Fukayosi kule Bagamoyo wakazi hawa wamekutwa na lita 75 za mafuta ya transfoma, kesi bado iko kwenye upelelezi’’
9. ‘’ 17 mwezi wa tatu, mkuranga huko na kwenyewe mtu mwengine ameenda, transfoma nne zenyewe wameenda kuzichukua kesi iko mahakamani’’
10. ‘’ ukienda chalinze wamekutwa na Nyaya za aluminium ambazo zilikuwa ni mali ya ETDCO na kwa kweli hapa na penyewe kuna mtu mmoja mdau wa ETDCO ndio mtengeneza mchongo’’.
11. ‘’ Sasa juzi tumeenda kumpekua mtuhumiwa mmoja juzi tu hapa tarehe 25 sitaki kumtaja wamemkuta na vitu vya Tanesco nyumbani kwake, mita anazo nyumbani, ana lakiri (seals) nne na zina namba ya shirika, huyo bwana maeneo ya chanika kule akakutwa na lakiri (seals) 221 zenye nembo ya shirika, amekutwa na rimoti units 37 , hawa watu wote wana connection na watu waliomo ndani ya shirika’’
‘’Sasa katika mazingira kama haya iko michongo mingine ambayo wafanyakazi wetu ndio wanashirikiana na wahalifu hawa’’. Amesema Dkt. Biteko
‘’sasa ninafahamu kuwa wapo wengine wapo mahakamani wapo wengine wako kwenye upelelezi, lakini mimi najiuliza mfanyakazi wa shirika la Tanesco aliyekamatwa redhanded (kidhibiti mononi) na vifaa, ni kweli kuna taratibu za kipolisi na upelelezi unaendelea kwa sababu ni lazima kutafuta haki ya mtu. Wewe MD wa Tanesco, una Imani gani na mtu wa namna hiyo ambaye yeye alikutwa na gari anaiba waya, una Imani gani naye?, halafu unaniambia eti kuna taratibu za kiutumishi mpaka zikamilike’’. Ameongeza
‘’lakini haya majizi yote, awe na connection (maana one of the thing kinachosumbua hapa ni connection zenu za mjini hapa) hatuwezi kuendekeza connections za watu huku watu hawana umeme, haiwezekani. Hawa wote walio kwenye hii taarifa, wako kwenye upelelezi, kwenye utumishi wa umma huku waweke pembeni watasubiri mkondo wao wa kisheria huko utakavyokuwa unaendelea’’. Amesisitiza Dkt Biteko