Wanafunzi wa shule ya msingi kibwegere iliopo Mkoa wa Dar es salaam ,Wilaya ya Ubungo, kata ya Kibamba wapo kwenye hatari kubwa ya kupata magonjwa ya kuambukiza kutokana Uhaba wa Vyoo kwa jinsia zote mbili (Wasichana na Wavulana )
Baadhi ya Wazazi wa watoto wanao soma shule hapo wamelalamika kjwepo kwa tatizo hilo kwa muda mrefu na wanapouliza kwa wahusika hakuna majibu ya kueleweka
Shule hiyo yenye idadi ya wanafunzi zaidi ya 1200 kuanzia darasa la kwanza hadi la saba imekuwa na matatizo mbalimbali ikiwemo uhaba wa madati hadi kupelekea wanafuzi kukalia mifuko ya viroba wawapo darasani pamoja na hili la ukosefu wa vyoo ambavyo awali vilikuwepo vikiwa na idadi ya matundu 8 na sasa vimebomoka vibaya hadi kufikia kufungwa na kuto kutumika
Hata hivyo wazazi hao wanasema hali ni mbaya hasi sasa wanafunzi wanajisaidia porini na tulipofanya jitihada za kumtafuta Mwalimu mkuu msaidizi ambaye amekaimu kwasasa (jina limehifadhiwa) alithibitisha kuwepo kwa changamoto ya aina hiyo na alidai swala hili lipo kwenye ngazi ya wilaya na sababu ya kuchelewa kutatuliwa linatafutiwa bajeti ya ujenzi
“swala hili lipo kwenye levo ya Mnispaandiyo wanalishughulikia na nikweli ni la muda na hii ni kwasababu walikuwa wana litafutiwa kifungu yaani bajeti “mwalimu alisema
Nao wazazi wakiongea na mwandishi wetu kwa nyakati tofauti walisema
“jitihada tumefanya kuongea na walimu na ili waweze kutusaidia lakini hatujapata chochote ,muafaka wowote hatujapata kwasababu kila mwalimu anamtupia lawama mwenzie anasema ye sio kazi yake ,kazi yake ni kufundisha “ mmoja ya wazazi alisema
“kiukweli kama juzi nimemuona mototo anatoka kujisaidia vichakani ni wakiume lakini nilipohojiana nae akasema choo chao ni kibovu kwahiyo ndugu mwandishi watoto wetu wana jisaidia vichakani” mmoja ya wazazi alisema