Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) na Shirika la Mawasiliano la Burundi (BBS ) zimetiliana Saini hati ya mkataba wa Kibiashara Wenye lengo la kuongeza huduma kwenye Mkongo wa mawasiliano.
Mkataba huo wa Mawasilano wenye thamamani ya Dola za Kimarekani millioni 3.3 sawa na Billion 8.3 za Kitanzania unalenga kuboresha sekta ya Mawasiliano sambamba na uboreshwaji wa Matumizi ya Mkongo wa taifa baina ya Nchi ya Tanzania na Burundi na Ukanda wa Afrika Mashariki (EAC) sambamba na Ukanda wa nchi zilizokusini mwa Afrika
Akizungumza katika Hafla ya utiliaji Saini Makubaliano hayo Februari 23 ,2024 jijini Dar es Salaam Waziri wa Habari Mawasiliano na Tenknolojia ya Habari Mhe. Nape Nnauye amesema kuwa utiliaji sani kati ya Shirika la Mawasiliano la Burundi BBS na TTCL Kutaongeza ushirikiano baina ya Tanzania na Burundi na kuongeza Soko jipya la kibiashara.
“Serikali ya Awamu ya sita imelenga kukuza Sekta ya Mawasilino kwa kuimarisha Huduma za Mkongo wa Taifa ilikuweza kukuza Uchumi wa kidigitali”asema Waziri Nape
Waziri Nape amesema kuwa utiliaji saini wa makubaliano hayo unalenga kufungua milango ya uwekezaji kati ya Tanzania na Nchi jirani.
Amesema kuwa ni vyema wananchi wote wa ukanda wa Afrika kuweza kujiunga na mkongo ili kuweka Mazingira bora ya Mawasiliano.
“Tunatoa Wito wa nchi zote za Bara la Afrika kuweza kujiunga na Mkongo huu wataifa ili kuweza kufanya Mawasiliano kwa urahisi zaidi”ameeleza Waziri Nape
Kwa upenda wake Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania TTCL Mhandisi Peter Ulanga Peter Ulanga amesema tukio hilo linakuza mahusiano ya kidiplomasia kati Tanzania na Burundi .
Amesema Mahusiano ya nchi hizo imekuwa ni nyenzo muhimu ya mashirikiano ya kiuchumi.
“Wateja wetu mmeona nguvu kubwa ambayo imekuwa ikiwekezwa katika kuboresha shirika”amesema Ulanga.