- Leah Ulaya aliyeteuliwa ukuu wa wilaya na Rais Dkt. Samia akaukataa uteuzi aapa kushinda kwa kishindo
- Makamu wake Suleiman Mathew Ikomba amvaa, aamua kugombea nae urais
- sasa mchuano ni Rais dhidi ya Makamu wake mfano wa Mbowe na Lissu walivyotoana jasho uchaguzi Chadema
- Mkutano mkuu wa uchaguzi wabadilishwa tarehe na sasa itafanyika juni 8 na juni 9
- vikao vya maandalizi ya uchaguzi huo vyapamba moto
- walioshindwa nafasi za mikoani wilayani waandaa mazengwe
- msimamo wa Leah Ulaya kwa uteuzi wake aliomgomea rais Samia wazua mjadala kuuelekea uchaguzi
Na. Mwandishi wetu,

Ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Leah Ulaya, Mwalimu wa shule ya msingi na rais wa chama cha walimu nchini CWT aliyeingia katika rekodi ya aina yake ya kuteuliwa ukuu wa wilaya na Rais wa nchi Dkt. Samia Suluhu Hassan na kuugomea uteuzi huo ili aendelee kuwa rais wa chama hicho bila kujali kuwa kufanya hivyo ni kuikosea heshma mamlaka kuu ya uteuzi nchini
Leah ulaya ambaye aligoma kwenda kituo cha kazi sambamba na aliyekuwa katibu mkuu wake Japhet Maganga ambaye baadae aliishia kutimuliwa kazini kwa utovu wa nidhamu amejotosa tena kugombea nafasi hiyo ya urais wa CWT safari hii akishindana na walimu wengine 17
Miongoni mwa wagombea waliojitokeza kugombea nafasi hiyo ni makamu wa Rais wa sasa wa chama hicho mwalimu Suleiman Mathew Ikomba ambaye kujitokeza kwake kugombea kunatajwa kuwa mwiba mkali kwa ulaya kutokana na mambo kadhaa wa kadha
Gazeti hili limewahi kuandika kwa undani juu ya matendo ya utovu wa nidhamu ya viongozi hao na kuzua mijadala mikubwa katika jamii hususani kada ya walimu na watumishi wa umma ambao kwao ni mwiko kugomea maelekezo ya kiongozi wa juu

Uchaguzi mkuu wa chama cha walimu nchini unataraji kufanyika katika mkutano mkuu wa chama hicho tarehe 8 na 9 mwezi huu mkoani Dodoma katika ukumbi wa mikutano wa Jakaya Kikwete huku mikutano ya awali kuelekea uchaguzi huo ikiwa tayari imeanza
“Tunaisubiri kwa hamu kubwa hiyo tarehe 8 na 9 tuelezane maana hasa ya kuwa mwalimu na heshima ya mwalimu katika jamii hasa kwenye maadili ya kiuongozi na kuheshimu mamlaka”. Amesema mmoja wa wajumbe wa KUT wa chama hicho
“unajua walimu tupo wengi sana hapa nchini, na kwa miaka kadhaa tumekuwa tukidai haki na maslahi yetu kwa vurugu bila mafanikio, tunapopata serikali inatusikiliza bila kelele ni wajibu wetu kuwa na viongozi wanaoweza kuimarisha mahusiano”. Ameongeza
Amesisitiza kuwa chama cha walimu sio chama siasa wala kikundi cha harakati, hivyo aina ya viongozi wanaohitajika ni wale wanaoweza kukaa meza moja na waajiri na kutatua changamoto za walimu

Jitihada za kumtafuta Leah ulaya na wagombea wengine zinaendelea