BAJETI YA WIZARA YA NISHATI YAGUSA KILA ENEO
NA MWANDISHI WETU
NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt.Doto Biteko ameliomba Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuidhinisha Bajeti ya Wizara ya Nishati kwa mwaka 2025/2026 ya kiasi cha shilingi Trilioni 2.2 ambapo asilimia 96.5 ya Bajeti yote ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo na asilimia 3.5 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.








