BALOZI NCHIMBI ATEMBELEA NYUMBANI KWA BABA WA TAIFA
NA MWANDISHI WETU
KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, kijijini Mwitongo na kukabidhiwa fimbo maalum na familia hiyo ya mwasisi wa Tanzania na CCM.










