MSIMAMO MKALI
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI wa Kilimo,Hussein Bashe amepiga marufuku rasmi bidhaa zote za kilimo kutoka nchini Afrika Kusini na Malawi kuingia nchini.
Uamuzi huo umekuja baada ya Bashe kuzipa siku saba serikali za nchi hizo kutengua uamuzi wao wa kuzuia bidhaa za kilimo kutoka Tanzania lakini zimegoma kufanya hivyo.











