MAJALIWA: ZAWADI YA DK. SAMIA NA DK MWINYI NI KUWAPA ‘MITANO TENA’
NA MWANDISHI WETU
WAZIRI MKUU wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa, amesema kuwa zawadi pekee ya thamani kwa Rais Samia Suluhu Hassan na Rais Hussein Mwinyi kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya michezo, sanaa na utamaduni ni kuwachagua tena kwa miaka mitano mingine, maarufu kama mitano tena.













