KISHINDO CHA DK. SAMIA
NA MWANDISHI WETU
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ameendelea kuwa kinara kufuatia ndoto zake za kukamilisha utekelezaji wa mradi wa Kufua Umeme wa Bwawa la Julius Nyerere (JNHPP) wenye uwezo wa kuzalisha megawati 2,115 kukamilika. Hayo yamebainishwa Rufiji mkoani Pwani wakati Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko alipotembelea mradi huo.













