WASIRA AKEMEA MAKUNDI CCM
NA MWANDISHI WETU, ITILIMA
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Stephen Wasira amewataka wanachama kuacha makundi kwa kuwa yanasababisha kushindwa katika baadhi ya uchaguzi, hivyo amesisitiza umoja na mshikamano. Amesisitiza kuwa, ukiona upinzani umeshinda katika ubunge au udiwani ushindi huo unatokana na makundi jambo ambalo husababisha wana CCM kumpigia kura mpinzani.











