Mkuu wa mkoa wa Simiyu Mhe. Kennan Kihongosi Jana akihutubia walimu katika ukumbi wa Kusekwa Memorial School kwenye ziara ya kutatua changamotoa za walimu mkoani Simiyu amempongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia kufanyika kwa ziara hiyo kutatua changamoto za walimu nchini.
“nimpongeze mheshimiwa rais Dktari Samia Suluhu Hassan kwa kuridhia hili jambo lifanyike kwasababu tunajua ridhaa yake ndo imetekeleza hilijambo kuwepo siku ya leo pengine asinge ruhusu hilijambo lisinge fanyika”. Amesema Kenan
Aidha aliwakumbusha walimu wajibu wao wa kwanza katika ziara hiyo iwe ni kuzungumza yale ambayo yana wasibu kwasababu ni fursa ambayo hutokea kwa nadra.
“Wajibu wenu wa kwanza walimu walimu wetu watumishiwenzetu wa Umma muwe huru kuzungumzayale ambayo yanawasibu, yale ambayo ni changamoto za binafsi au za kitaasisi semeni kwasababu fursa kama hii hamtaipata wakati mwingine” Amesema Kenan
Vilevile aliwasihi kusema ukweli katika kufikisha changamoto zao hatakama ukweli huo unamgusq yeyote katika watumishi na viongozi wao kwasababu wajibu wao ni kusema ili viongozi wapate majibu ya chanagamoto zao.
“Na katika kuzungumza ukweli huwa hakuna gharama msiogope kusema ukweli hatakama unamgusa peyote aliyeko hapa mbele wajibu wenu ni kusema ili viongozi hawa waweze kuwa na majawabu kamili na wajue wanaenda kushughulikia jambo gani”. Amesema Kenan
Pia aliwakumbusha na kuwasisitiza juu ya uwajibikaji ili kutimiza lengo la kuwahudumia wananchi.
“Niwaombe sana lengo lilelile ambalo likikusukuma ukaomba ajira basi lengo hilo liendw likatekelezeke katika kuwahudumia wananchi” Amesema

kshwaw