Mzigo wa Uongozi: Hapo awali alikuwepo Rais aliyekuwa akiitwa Mweta katika taifa la Uvanga, alikuwa na sifa ya uzalendo na kupenda wananchi kulingana na hata pengine kuzidi upendo wa familia yake.
Rais Mweta alikuwa kiongozi mwenye upendo na kujitolea kwa nchi yake ya Uvanga.
Alikuwa na ndoto kubwa ya kuleta maendeleo na ustawi kwa wananchi wake. Lakini, kama Rais, alikabiliana na majukumu mengi magumu na changamoto kubwa.
Moja ya majukumu magumu zaidi ya Rais Mweta ilikuwa kufanya maamuzi magumu. Alikuwa na jukumu la kuamua kuhusu masuala muhimu ya nchi, kama vile uchumi, usalama, na afya. Maamuzi haya mara nyingi yalikuwa magumu na yenye athari kubwa kwa maisha ya watu lakini hayakuacha kumfanya aonekane mbaya.
Alitokomeza ufisadi, rushwa ubadhilifu nakujenga miundombinu bora lakini bado walimsema kwa ubaya kwa sifa yake ya kuwa mzalendo wa kweli.
Mbali na kupigania wananchi kwa kuwaletea maendeleo ya ndani, Rais Mweta alihangaika kwa kujenga uhusiano wa kimataifa ili kusogeza fursa kwa wananchi wake
Rais Mweta alipata uzoefu wa upweke wa uongozi kwani Mara nyingi alikuwa peke yake katika kufanya maamuzi magumu. Alikuwa na washauri na wasaidizi, lakini hatimaye, uamuzi ulikuwa wake. Hii ilikuwa changamoto kubwa kwake, na ilimfanya ahisi mzigo mkubwa wa uwajibikaji huku chuki zikizidi juu yake.
Rais mweta alikuwa na familia ndogo, mke na watoto wawili. Lakini, kwa sababu ya majukumu yake mengi, hakuipa familia yake kipaombele zaidi na alikuwa na muda mdogo wa kuwa na familia yake.
Alikosa sherehe nyingi za kuzaliwa, maadhimisho ya shule, na hata wakati mwingine alikosa chakula cha jioni na familia yake.
Japo ilimuumiza sana, lakini alijua kwamba alikuwa na jukumu kubwa la kutumikia nchi yake kwa uzalendo.
Mbali na yote anayofanya kwaajili ya wengine Wakati mwingine, Rais Mweta alifanya maamuzi ambayo hayakueleweka na watu.
Alijaribu kukusanya kodi kwa wingi ili kuboresha miundombinu lakini Watu walimkosoa na kumshutumu kwa kutowajali.
Hii ilikuwa changamoto kubwa kwake, lakini alijua kwamba alikuwa akifanya kile alichoamini kuwa ni sahihi kwa nchi yake.
Aliwahi kuwasihi wananchi wake wayapokee anayoyafanya kwani yana manufaa makubwa kwa badae yao lakini walimpa mpaka jina la bwana haambiliki.
Kauli ya “nikifa mtanikumbuka” baada ya kufariki kwake kila mmoja aliikumbuka na kuchapisha katika mitandao ya kijamii na kumuita shujaa walie muita Bwana haambiliki.
Mmmmmmh! Rais ni kazi ngumu na yenye changamoto nyingi. Rais anapaswa kuwa na ujasiri, hekima, na upendo kwa nchi yake. Anapaswa kuwa tayari kufanya maamuzi magumu na kukabiliana na upweke wa uongozi. Lakini, zaidi ya yote, anapaswa kuwa na moyo wa kutumikia wananchi wake na kuwaletea maendeleo na ustawi.
Mema aliyofanya Rais Mweta na bado alipigwa vita.
Je! ni nani anaweza kuongoza nchi kama bado walimuona hatoshi?