![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0011-1024x682.jpg)
ILE kadhia ya ukosefu wa maji kwa wakazi wa maeneo ya Tabata, Kinyerezi na Segerea sasa imefikia mwisho baada ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) kukamilisha mradi wa upelekaji maji kwa asilimia 99.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0018-1024x682.jpg)
Kaimu Mkurugenzi wa DAWASA,Mkama Bwire amewaeleza wananchi wa maeneo hayo kwamba kuanzia Februari 20 mwaka huu watafungulia rasmi maji ili kuwaondolea kero hiyo ya muda mrefu.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0005-1024x682.jpg)
Bwire alisema,serikali ya awamu ya sita chini ya Rais Dk.Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuwaondolea kero ya maji Wananchi wake kwa kutoa fedha za ukamilishaji miradi mbalimbali ikiwemo huo wa ambao unakwenda kuwa mwarobaini wa tatizo la maji kwa wakazi wa maeneo hayo.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0015-1024x682.jpg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0016-1024x682.jpg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0020-1024x682.jpg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0013-1024x682.jpg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20250208-WA0018.jpg)