KUNA wakati jarida maarufu la Forbes ilizua maoni mengi wakati lilipodai mmoja kati ya watu nyota kwenye mitandao ya kijamii kwa wakati huo, Kylie Jenner amepata utajiri wa karibu Dola bilioni 1.
Haya ni mafanikio ambayo watu wachache sana wanaweza kuyapata na kulikuwa na watu 5,700 kote duniani waliokuwa na utajiri unaozidi dola milioni 500 2017 kulingana na ripoti kutoka kwa Global Wealth Report. Mabilionea halisi hata hivyo ni wachache. Lakini mtu anahitaji nini hadi kuitwa bilionea?
ANZISHA KAMPUNI
Ukiangalia watu matajiri duniani kwa mfano Jeff Bezos wa Amazon, Mark Zuckerberg wa Facebook, Amancio Ortega wa Zara na Jack Ma wa Alibaba ndio wanatawala. Forbes inawatambua watu thuluthi mbili ya mabilionea 2,208 kuwa waliojizolea utajiri wao na idadi hiyo inazidi kuongezeka. Kylie Jenner kumshinda Mark Zuckerberg kwa kasi ya utajiri Ni kweli kuwa neno utajiri wa kujizolea linaweza kuwa na ugumu kulielezea.
Hatua ya Forbes kumtaja Kylie Jenner ambaye alizaliwa katika familia tajiri kama aliyejipatia utajiri ilizua maoni mengi kwenye mtandao.
PESA ZA URITHI
Karibu theluthi moja ya watu walio katika orodha ya Forbes walirithi pesa zao. Hao ni pamoja na watu saba wa familia ya Walton, warithi wa maduka wa Walmart na Francoise Bettencourt-Meyers ambaye familia yake ilianzisha kampuni ya L’Oreal. Mwanzilishi wa Amazon sasa ndiye mtu tajiri dunia.
Urithi ni muhimu hasa barani Ulaya kutokana na kuwa umechangia kwa karibu nusu ya mabilionea kulinda na takwimu za Forbes za mwaka 2014. K u n a s a b a b u k a d h a a zilizochangia watu ambao walirithi mali kuzidi kuongezeka. Sababu moja ni kuwa thamani ya mali kama hisa imeongezeka kwa haraka kuliko mali nyingine miaka ya hivi karibuni.
WEKEZA
Kuna zaidi ya watu 140 katika sekta ya fedha walio na utajiri unaozidi dola blioni 2.5 kwenye orodha ya watu matajiri. Bill Gates alichukua tena uongozi wa kuwa mtu tajiri duniani na wengi wao ni kutoka nchini Marekani ambapo asilimia 25 ya mabilionea hupata utajiri wao kutoka sekta ya fedha. Lakini usidhani kuwa ni rahisi kupata mafanikio hayo.
Mkuu wa kampuni ya JP Morgan Chase boss Jamie Dimon ni baadhi ya mabilionea wachache waliochukua mkondo huo. Na wafadhili wengi karibu asilimia 20 ya watu matajiri zaidi ya 143 wana uhusiano na mifuko ya uwekezaji. HAMA ULIPO Idadi ya mabilionea katika kila nchi inashuka, ila eneo linaloongezeka kwa watu matajiri duniani ni la Asia Pacific.
Karibu asilimia 29 ya watu mabilionea wapya mwaka uliopita walitokea eneo hilo kwa mujibu wa jarida la WealthX linalokadiria kuwa kuna mabilionea 2,750 duniani idadi iliyo juu kuliko ile ya Forbes. China pekee ina mabilionea 29 kati ya 259 mabilionea wapya, idadi ya juu kuliko ya nchi yoyote. Licha ya hatua zilizopigwa sehemu zingine duniani, Marekani inasalia nchi yenye mabilionea wengi zaidi ikiwa na mabilionea 585.
USIWE MTU WA KESI
Mabilionea si wageni kwa kesi mahakamani. Kwa mfano Bill Gates, anaweza kujulikana kama mtu tajiri wa kutoa misaada lakini historia yake si safi vile. M namo miak a ya tisini Marekani iliishtaki kampuni ya Microsoft kwa kutumia mbinu zinazozuia ushindani.
Serikali ya Marekani ilishinda na Microsoft ikakata rufaa. Kesi hiyo iliishia makubaliano. Tume ya Ulaya nayo ishaipiga faini kampuni ya Microsoft. Baadhi ya kampuni ambazo pia zimepigwa faini ni pamoja na Google na Samsung na pia zile zisizo za teknolojia kama ya kamari ya Las Vegas Sands.