KUNA fikra potofu zimejengeka miongoni mwa watu wakidhani kuwa kufanya kazi kwa bidii ni utumwa. Hii ni kutokana na dunia ya sasa kujaa watu wasiopenda kazi na wavivu.
1. Bidii inasaidia Kutumia Muda Vyema Huwezi kutumia muda vyema kama hutofanya kazi kwa bidii. Ukiwa na bidii katika kufanya kazi, unaweza kufanya kazi za siku nzima ndani ya saa moja au kazi za siku mbili ndani ya siku moja. Hakuna mtu yeyote aliyefanikiwa bila kutumia muda vyema; muda ni mali, hivyo yakupasa uutumie vyema kwa kufanya kazi kwa bidii.
2. Bidii inasaidia Kufikia Malengo Yako Kanuni moja wapo ya kufikia malengo ni kufanya kazi kwa bidii. Safari ya mafanikio siyo ya mteremko, inahitaji juhudi nyingi ili tuweze kuona matokeo. Hakuna mtu aliyewahi kufanikiwa kwa kufanya kazi kivivu; fuatilia watu waliofanikiwa watakueleza jinsi wanavyofanya kazi usiku na mchana ili kukamilisha ndoto zao.
3. Bidii inasaidia Kuheshimika Nani atamheshimu mvivu? Kwa hakika hakuna. Mtu anapokuwa mwenye bidii utasik ia k auli kama vile huyo hapendi mchezo, akishaingia kwenye kazi zake humpati, hageukagi nyuma kwenye kazi huyo, kama huyo yupo hiyo kazi lazima iishe, n.k. H i z i n i b a a d h i y a k a u l i zinazoonyesha kuheshimiwa kwa mtu husika kutokana na kufanya kazi kwa bidii. Ikiwa unataka kuheshimika ni lazima ufanye kazi kwa bidii.
4. Bidii inasaidia Kutambulika Ikiwa unafanya kazi kwa bidii huna haja ya kujikombakomba kwa wakubwa au mbele za watu ili utambulike; bidii yako ya kazi itakutambulisha. Naamini umewahi kusikia watu wakipewa tuzo kwenye sherehe za kitaifa kutokana na kufanya kazi kwa bidii; hili linatupa picha ya kipekee ya faida ya kufanya kazi kwabidii. Usijali hata kama wanakudharau au wanakuona duni, wewe fanya kazi kwa bidii watakutambua ukiwepo au hata wakati utakapoondoka wataona pengo lako.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/IMG-20231006-WA0093-980x653-1.jpg)
5. Bidii inasaidia Kuondoa Lawama Mara nyingi idara au ofisi zenye malalamiko mengi ni zile zenye wafanyakazi wavivu. Pia wafanyakazi wengi wanaolaumiwa na kunyoshewa vidole na waajiri wao, wengi ni wale wavivu. I l i k u e p u k a l a w a m a a u manung’uniko, ni vyema ukafanya kile unachokifanya kwa bidii kwani kwa njia hii utaongeza ufanisi wako.
6. Bidii inasaidia Kupata Matokeo Makubwa Hakuna matokeo makubwa bila kazi kubwa, yaani kazi iliyofanywa kwa bidii. Kwa mtu yeyote anayetaka kuona matokeo makubwa katika kile anachokifanya ni lazima kwanza afanye bidii. K u m b u k a h a t a m k u l i m a anayefanya bidii katika kilimo ndiye huvuna zaidi ya wakulima wengine. Hivyo kufanya kazi kwa bidii hakuepukiki kwenye maisha.
7. Bidii inasaidia Huleta Fursa Mpya Mtu mwenye bidii kila mara hufungua milango ya kupata fursa mpya, kazi zake na bidii yake humtangaza na kumfungulia fursa zaidi. Hakuna mtu atakayempa mtu mvivu kazi au fursa zenye manufaa.
8. Bidii inasaidia Kuboresha Afya Kukaa bila kufanya kazi ni kujiletea matatizo ya kiafya; kazi ni sehemu ya mazoezi. Hivyo kufanya kazi kwa bidii kutakufanya uwe mwenye afya njema kila wakati. Unalotakiwa kukumbuka hapa ni kuwa na kiasi, fanya kazi kwa bidii lakini usipitilize hadi uathiri afya yako.
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/cq5dam.thumbnail.cropped.750.422-1.jpeg)
![](https://jamvilahabari.co.tz/wp-content/uploads/2025/02/MJASIRIAMALI-1-1024x576.png)