Kukamilika kwa uwanja wa mpira wa kisasa wa Samia suluhu Academy utaongeza utalii wa kimichezo( Sports tourism).
Kauli hiyo imetolewa na Katibu wa NEC itikadi, uenezi na mafunzo CPA Amos makalla kwenye ziara yake ya kichama mkoa wa kusini Unguja.
Aidha mbali ya kukuza utalii kwa timu zote zitakazokuja Kizimkazi uwanja na chuo hicho utatumika kukuza vipaji vya wanasoka nchini.“Nawaona kina Fei Toto(mchezaji wa Azam) wengi tu watatoka hapa” alisema .
Uwanja wa Samia Suluhu Hassan utakuwa na uwezo wa kuingiza washabiki 23,000.