Mgawanyo wa majukumu na utii wa maelezo ya wataalamu ni sababu ya kufanikiwa kwa mambo mengi yanayohitaji utaalamu. Nikukumbushe kitu habari ya kusema “oya mwanangu nipigie kazi yangu huku ukipiga yako kuna nafasi kubwa ya kuharibukazi”. kitu kilichofanyika kwa maafisa trafiki wa ndege ya Amerikan Airline na kusababisha ajali
Na pia mungu alituagiza na kushusha andiko lisemalo “akhibalinas matuhibul-nafska” pendeni watu kama mnavyopenda nafsi zenu.
watu wata angamia endapo kilamtu atakua anafanya mambo kwa maslahi binafsi pasi na kujali ubinadamu unataka nini hivyo tunapaswa kujali nafsi za wengi kabla ya sisi wenyewe, kitu kilicho kosekana kwa rubani wa healkopta ya kijeshi na kupelekea ajali.
Huu ni mkasa wa kuanguka kwa ndege ya shirika la american airline huko marekani baada ya kugongana na helikopta ya kijeshi. Na mkasa huu umesababishwa na uzembe wa kitego cha trafiki ya ndege na rubani wa helkopta ya kijeshi kutokufata maelekezo na njia aliyopangiwa.
Iko hivi. “Mdhibiti wa trafiki wa anga aliruhusiwa kuondoka kwenye kituo chao muda mfupi kabla ya ndege ya American Airlines Flight 5342 kugongana angani na helikopta iliyokuwa ikitokea Washington DC.Hayo ni kwa mujibu wa wadadisi wa mambo waliozungumza na The New York Times na ripoti ya ndani ya FAA ambayo imeanza kuchunguza mkasa huo ulioua watu 67.
Mdhibiti wa trafiki wa anga katika Reagan National aliachwa kushughulikia trafiki ya helikopta na kusimamia ndege jukumu ambalo lingepaswa kuwa jukumu lililogawanywa. Imeibuka pia kuwa helikopta ya Jeshi, iliyokuwa imebeba wanajeshi watatu, waliohusika katika mgongano huo inaweza pia kuwa imekengeuka kutoka kwa njia yake iliyoidhinishwa.
Kituo hicho kilizungumza tena na watu wa ndani ambao walisema Black Hawk haikuwa kwenye njia yake iliyoidhinishwa na inaruka juu zaidi kuliko ilivyopaswa kuwa. Uidhinishaji ulikuwa umetolewa kwa helikopta hiyo kuruka umbali usiozidi futi 200 upande wa mashariki wa Mto Potomac, ambapo ingeepuka ndege ya abiria.
Rubani wa helikopta hiyo alithibitisha kuona ndege ya shirika la ndege la American Airlines na kuambiwa washike njia waliyopangiwa na kwenda nyuma ya ndege hiyo. Vyanzo vya habari vilisema rubani hakushikamana na njia hata hivyo na alikuwa umbali wa maili nusu na vile vile alikuwa kwenye mwinuko wa futi 300”.