KIKWAZO cha wengi kuingia kwenye biashara kimekuwa ni mtaji, hiki kimekuwa kilio cha kila anayetaka kuingia kwenye biashara na akashindwa au aliye kwenye biashara na kushindwa kuikuza.
Kila anayeshindwa kuingia kwenye biashara au aliye kwenye biashara na kushindwa kuikuza, sababu yake kuu huwa ni kukosa mtaji. Lakini mimi nimekuwa nawaeleza watu ukweli huu, kukosa mtaji hakujawahi kumzuia mtu mwenye nia ya kweli kuingia kwenye biashara.
Bali kukosa mtaji ni sababu rahisi kwa yeyote kutumia, ambayo hakuna anaweza kukukatalia. Naamini bila ya shaka yoyote kwamba mtu yeyote anaweza kuanzisha na kukuza biashara yake hata kama hana kabisa mtaji wa kuanzisha biashara hiyo.
Nina ushahidi kwangu binafsi na ushahidi kutoka kwa wengine wa jinsi gani hilo linawezekana na leo nakupa nafasi ya wewe kujua hili, ili uache kutoa visingizio na uanzishe au kukuza biashara yako.
AINA ZA MITAJI Watu wengi wanapozungumzia mtaji wa biashara, huwa wanazungumzia aina moja tu ya mtaji, ambayo ni mtaji fedha. Wakikosa aina hii ya mtaji, wanaona hawawezi kuingia kwenye biashara. Usichojua ni kwamba kuna aina tano za mtaji wa kuanzisha biashara, fedha ni moja ya aina hizo, ila kuna aina nyingine 4 ambazo ukijua jinsi ya kuzitumia vizuri utaweza kuanzisha biashara.
Ninachotaka kukuambia hapa ni kwamba, hata kama huna fedha, kuna aina nyingine za mtaji unazo katika hizo tano, hivyo usikate tamaa na kujiambia kwa kuwa huna mtaji basi huwezi kuingia kwenye biashara.
VYANZO VYA MTAJI FEDHA Inapokuja kwenye mtaji fedha, wengi wanaokwama kupata mtaji huu huwa wanahangaika na njia moja tu, na wengi ni njia ya mkopo. Utawasikia wengi wakisema sina sifa ya kukopesheka, hivyo siwezi kupata mtaji wa kuanza biashara. Hili pia siyo sahihi, kwa sababu vyanzo vya mtaji wa fedha siyo mkopo pekee.
Kuna vyanzo vikubwa vitano vya kupata mtaji wa fedha kwenye biashara, mkopo ni moja kati ya njia hizo tano na ambao una vikwazo vingi. Kuna vyanzo vingine vya kupata mtaji fedha, tena ambavyo ni rahisi na visivyokuumiza kama kilivyo chanzo cha mkopo. Ulivijua vyanzo hivyo na jinsi ya kuvitumia vizuri, utaweza Huwa wanasema pesa huleta pesa lakini wakati mwingine inaweza kuwa tofauti hasa pale unapotaka kuanzisha biashara unaweza ukaanza hata kama hauna pesa au una mtaji mdogo.
Yafuatayo ni mambo manne unapaswa kuyazingatia. Tunza kidogo kidogo Je hauna pesa ya kutosha ili kuanzisha biashara yako, kuwa na subira. Njia rahisi ni kutunza pesa kidogo kidogo kila wiki au hata kila mwezi mpaka pale utakapopata pesa ya kutosha kuanzisha biashara, kwa kufanya hivi kutakuepusha kuingia kwenye madeni.
Asilimia flani ya faida utakayoipata unaweza kuiongezea kwenye biashara yako ili kuisaidia ikue. Angalia fursa zinazokuzunguka Kama utaangalia kwa makini utagundua mara nyingi tunazungukwa na fursa kibao zinazoweza kutuingizia kipato cha ziada. Na unaweza kuanza kutunza kiasi hiki cha pesa utakachokipata ili kikusaidie kufungua biashara.
Kitu cha kwanza kabisa unaweza kuwajulisha majirani zako kwamba unatafuta kazi ili kama watapata taarifa kuhusu kazi uwe wa kwanza kuambiwa. Tumia ujuzi ulionao Je! umewahi kufikiria kuhusu kubadilishana ujuzi? Badala ya kuazima pesa au kununua kifaa chako binafsi, Angalia mazingira yanayokuzunguka. Yawezekana yakakuruhusu kubadilishana kitu kati ya muda, ujuzi na hata vifaa.
Labda ngoja nikupe mfano; labda unahitaji cherehani ili kushona bidhaa unazohitaji kuziuza, unaweza kuazima cherehani kwa jirani yako na badala yake unaweza kuwaahidi kuwa utawasaidia kazi zao pale watakapokuhitaji kufanya hivyo. Kitu cha kwanza ainisha ujuzi na vifaa unavyovihitaji ili kuanzisha biashara yako kisha omba msaada kwa watu wanaokuzunguka.
Utashangazwa na jinsi unavyoweza kufanikiwa kirahisi pasipo kuhitaji pesa. Usiogope kuulizalabda wanaweza kukataa ila sio mara nyingi na siku zote watafurahia kukusaidia. Tangaza biashara yako mdomo Wanafamilia na hata marafiki zako ni njia nzuri sana ya kutangaza biashara yako. Waombe marafiki zako wawaambie marafiki na jamaa zao kuhusu biashara au huduma unazozitoa au hata wanaweza kukusaidia kutangaza kupitia mitandao yao ya kijamii.
Mapendekezo binafsi kutoka kwa watu na pale wanapoizungumzia biashara yako vizuri itaisaidia mno kukua na kukuza jina lako na baada ya muda utashangazwa na jinsi taarifa zinavyosambaa haraka kwa njia ya kuambizana. Kumbuka, sio lazima kuwa na pesa nyingi ndipo uanzishe biashara. Kuwa mbunifu, tazama fursa zinazokuzunguka,na tumia ujuzi na rasilimali walizonazo watu wanaokuzunguka ili kuanzisha biashara.
Omba msaada kutoka kwa wanafamilia na marafiki ili wakusaidie kutangaza biashara yako nakwambia utashangaa jinsi utakavyofanikiwa pasipo kuhitaji pesa