Leo kwenye mkutano wa wakuu wa afrika kujadili nishati unaofanyika jijini Dar es salaamu katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere International Convetion Center (JNICC) Naibu Waziri mkuu wa Tanzania Mhe.Dkt. Doto Mashaka Biteko ameeleza dhamira ya mkutano huo ni kuhakikisha kufikia 2030 waafrika milioni 300 ambao bado hawana umeme wanakuwa na umeme.
Aidha ameweka wazi idadi ya waafrika takribani 571 bado hawajafikiwa na huduma ya nishati ya umeme huku mkutano huo unalenga kufikia matarajio ya kupunguza idadi hiyo ndani ya miaka mitano kwa kuwafikia waafrika wapatao 300
“Pamoja na mafanikio makubwa ya kuzalisha umeme barani Afrika, takriban Waafrika milioni 571 bado hawana huduma ya umeme. Mkutano huu umeitishwa rasmi kwa lengo la kujadili namna ya kuongeza upatikanaji wa umeme kwa watu milioni 300 barani Afrika katika kipindi cha miaka mitano ijayo” Amesema Biteko.
Vilevile ameeleza mkutano huo utawapa fursa mawaziri wa nishati, viongozi wa taasisi za kimataifa za kifedha, wataalamu na mashirika ya kiraia, watapata fursa ya kujadili na kukubaliana malengo ya kuhakikisha vipaombele vya sera suluhisho, na ahadi za jinsi ya kutekeleza mpango wa mission 300.
“Katika mkutano huu, Mawaziri wa Nishati, Viongozi wa Taasisi za Kimataifa za Kifedha, Wataalam na Wadau wa Mashirika ya Kiraia, watapata fursa ya kujadili na kukubaliana malengo, vipaumbele vya sera, suluhisho, na ahadi za jinsi ya kutekeleza Mpango wa Mission 300” Amesema Biteko.
Aidha Dkt. Biteko ameeleza mkutano huo ni kichocheo cha utekelezaji wa sera ya taifa ya nishati yenye lengo la kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi ambapo sera hiyo ina malengo ya upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati na kuongeza mchango wa nishati mbadala nchini.
“Tanzania inachukulia mkutano huu kama kichocheo cha utekelezaji wa Sera yake ya Taifa ya Nishati inayolenga kuendeleza nishati endelevu, uhifadhi na ufanisi. Sera hiyo pia inalenga kuongeza upatikanaji wa huduma za kisasa za nishati na kuongeza mchango wa nishati mbadala katika mchanganyiko wa uzalishaji ili kuimarisha upatikanaji, uhakika na usalama wa nishati” Amesema Dkt. Biteko.
Pia ameeleza jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha suluhisho la upatikanaji wa nishati safi ya kupikia inapatikana barani afrika.
“Rais Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele katika kukuza upatikanaji wa suluhisho la nishati safi ya kupikia barani Afrika. Jitihada hizi zimeungwa mkono na mkakati wa kitaifa na yamejumuishwa katika Azimio litakalotiwa saini, huku tukitoa wito wa ahadi na ushirikiano zaidi katika kuboresha upatikanaji wa suluhisho la nishati safi ya kupikia barani mwetu” Amesema Dkt. Biteko.
Vilevile baadhi ya viongozi waliohudhuria katika mkutano huo kutoka katiaka mashirika tofauti tofauti walizungumza juu ya mkutano huo na nchi mwenyeji wa mkutano.
Rais wa benki kuu ya dunia Bwn. Ajay Banga akizungumza mapema katika mkutano huo ameeleza uwezekano wa kubadilisa sura ya afrika kwa kuunganisha rasilimali zilizopo na kuwa na juhudi za Pamoja
“Tunaweza kubadilisha sura ya Afrika kwa kuwa na juhudi za pamoja za kuunganisha rasilimali zilizopo kuhakikisha nishati ya umeme inawafikia wananchi wengi zaidi Afrika ifikapo 2030” Amesema Bwn. Ajay
Halikadhalika Rais wa Benki ya Maendele ya Afrika (AFDB), Dkt. Akinumwi Adesina ameeleza Tanzania ni taifa la kuigwa katika uwekezaji wa miundombinu ya umeme kwakua miongoni mwa mataifa yaliyopiga hatua kwa kusambaza umeme katika vijiji vyake vyote.
“Tanzania imekua mfano wa kuigwa kwa kufanya vizuri katika uwekezaji wa miundombinu ya umeme kwa kuwafikishia nishati ya umeme wananchi katika vijijini vyote 12,318” Amesema Dkt. Adesina.