Leo katika viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kwenye mkutano wa kumkaribisha makamu mwenyekiti wa chama Cha mapinduzi Stephen Wasira amewataka wana CCM kuchagua viongozi wanaokubalika kwa jamii ili kutimiza lengo la chama la kushika dola.
Ameyasema hayo wakati akirejelea ajenda za mkutano mkuu uliofanyika jijini dodoma, katika kipengele Cha wanaostahili kupiga kura ili kupata viongozi watakao wakilisha chama, mara baada ya mabadiliko ya katiba na kuruhusu kamati za utekelezaji kwenye matawi kushiriki kupiga kura .”Sasa ombi langu kwa vikao vya chama sasa tulete watu wanaoweza mamaana tatizo letu huyu ni mwenzetu nani asiekuwa mwenzetu wote ni wenzetu”.
Na alisisitiza kwa kusema “na kama mwenzetu ana sifa zaidi kuliko mwenzetu basi mlete mwenzetu mwenye sifa zaidi maana chama hiki hatuwezi kuletewa mtu hakubaliki alafu kazi yetu iwe kusukuma maka tunasukuma jiwe” Amesema Wasira.
Vilevile ameeleza juu ya miradi iliyo achwa na rais wa awamu ya tano Hayati Dkt. John Magufuli ikitimia chini ya serikali ya awamu ya sita ya Raisi Dkt. Samia Suluhu ametimiza baadhi ya miradi hiyo ikiwa ni mradi wa treni ya umeme, bwawa la Nyerere kwaajili ya kufua umeme huku akieleza maendeleo aliyopatikana katika sekta ya uchumi,elimu, afya na maji chini ya Dkt. Samia Suluhu.
Lakini pia Makamu mwenyekiti wa chama cha mapinduzi akihutubia ameeleza wale wanaohoji juu ya chama cha mapinduzi kukaa muda mrefu madarakani kwa kuwaambia wanakazi ya kufanya ndomana wameshika dola muda mrefu.
“Tumekaa muda mrefu kwasababu tuna kazi ya kufanya” wasira
Aidha Makamu mwenyekiti ametoa historia fupi ya jijila dar es Salaam kuhusu umeme huku akilinganisha zamani na maendeleo ya sasa yaliyoletwa na CCM.
“Dar es Salaam hakukua na umememe” Wasira
Makamu ameeleza maendeleo yaliyoletwa na chama cha mapinduzi nimakubwa huku akitolea mfano wa miaka ya sitini kulikuwa na barabara tatu za lami tanzania nzima na sasa CCM ikiwa sababu ya barabara mpaka za mitaa kuwa na laminate.
“Kulikuwa na barabara tatu tuu za laminate tanzania” wasira
Vilevile ameeleza kuwa atakaesimama na kusema CCM hamna lolote katika kila hatua ya nchi watawaambia wao ndo hawana lolote.
“Ukisimama na kusema hamna lolote tunakuambia wewe ndio sio chochote”.
Pia ameweka wazi juu ya dhamira kuu ya chama cha mapinduzi ni kukamata dola huku akieleza sababu chama cha mapinduzi kina kazi ya kufanya.
“Dhamira ya chama cha mapinduzi ni kukamata dola kwasababu tuna kazi ya kufanya”
Haya yote ni marejeo ya vikao vikuu vya chama Cha mapinduzi na mkutano mkuu ulio fanyika Dodoma ili kuweka sawa na kuimarisha nguvu ya chama na kitekeleza lengo kuu la kushika dola na kupata viongozi watakao fanikisha kutimiza ilani ya chama