WAZIRI w a Nchi,Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, George Simbachawene amemshukia aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA)Freeman Mbowe kuhusiana na hoja yake aliyoitoa ya kubeza juhudi ya Serikali ya kutaka kuondoa umaskini wa watu kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwa kuwagawia fedha.
Simbachawene ameyasema hayo mara baada ya kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo iliyotekelezwa kupitia TASAF Mkoani Singida ambapo amesema TASAF ni mpango mmojawapo wa uwezeshaji wananchi kiuchumi lakini Serikali ina mipango lukuki.
“Jana (juzi) nilikuwa nasikiliza ule Mkutano wa Uchaguzi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) nilimsikia Mbowe wakati akitoa taarifa ya Chama hicho kuwa “Serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) inataka kuondoa umaskini wa watu kupitia TASAF kwa kuwagawia fedha”
“Ni kweli Serikali ya CCM inataka kuondoa umaskini wa watu wake hasa wale wasiojiweza kabisa kwa kuwasaidia kifedha lakini pia Serikali hii inatumia mfuko wa TASAF kuondoa changamoto zinazogusa maisha ya wananchi moja kwa moja kwa kwenda kurekebisha miundombinu pamoja na vikwazo katika maisha yao ikiwemo ujenzi wa vivuko ili waweze kwenda mashambani kwa urahisi hususani wakati wa msimu wa mvua” amesisitiza Simbachawene Pia,
Simbachawene amesema Serikali kupitia TASAF imekuwa ikijenga vituo vya afya mahali ambako kuna zahanati zisizokidhi mahitaji ya wananchi ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya lengo likiwa ni kupambana na umaskini “Nataka nimwambie Kaka yangu Mbowe kwamba TASAF ni mpango mmojawapo wa kuwezesha wananchi wetu kiuchumi lakini Serikali yetu ina mipango mingi sana na tunayo Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi” amesisitiza Mhe.
Simbachawene Amesema Serikali ina Mfuko wa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi ambapo kuna njia mbalimbali za kuwagusa kiuchumi ikiwemo vijana na makundi mbalimbali lengo likiwa ni kupambana na umasikini na kuwapa ahueni katika hali zao za maisha Vijana na Viongozi wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wakiongozwa na Mwenyekiti wao Mohammed Kawaida na Katibu Mkuu Jokate Mwegelo wamesema wako tayari kuhakikisha Wagombea wa nafasi ya Urais waliopitishwa na Mkutano Mkuu wa CCM 2025, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi, wanashinda kwa kishindo.
Mwenyekiti wa UVCCM Mohammed Kawaida amesema hayo baada ya Vijana kufanya matembezi ya hisani katika Jiji la Dodoma ikiwa ni kuunga mkono maamuzi ya Wajumbe wa Mkutano Mkuu uliofanyika January 18 na 19,2025 na kuwapitisha Dkt.Samia na Dkt. Mwinyi.
Kwa upande wake Katibu Mkuu wa UVCCM Jokate Mwegelo amesema matembezi hayo ni ahadi walioiweka ili kuunga mkono maamuzi ya Wajumbe na hivyo wako tayari kuhakikisha adhima ya kuhakikisha Chama kinaendelea kushika Dola ipo mikononi mwa Vijana kwani Mgombea mwenza wa Urais kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Emmanuel John Nchimbi ni zao la UVCCM.
Zaidi ya Vijana 1000 wakiwemo Wanafunzi wa Vyuo na Vyuo Vikuu, baadhi ya Wenyeviti wa Mikoa na Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Vijana Ng’wasi Kamani wameingia barabarani na kupitia Mitaa mbalimbali ya jiji la Dodoma kufanya matembezi hayo