
WAPO NANE! Imeelezwa Manchester United kuna wachezaji nane ambao hawana sifa za kuichzea timu hiyo, huku ikidaiwa hata ufikaji wao hapo inabidi ‘waulizwe kwa makini’ wale waliowaleta.
Kauli hiyo imetolewa na mchezaji wa zamani wa timu hiyo, aliyepita katika mafanikio makubwa Paul Scholes, ambaye alisema wachezaji hao wanapaswa kuuzwa na timu kutengenezwa upya.
Paul Scholes amesema, wachezaji hao nane wanatakiwa kuuzwa kwa haraka mno kabla ya dirisha la sasa la usajili kufungwa, la sivyo timu itaendelea kufanya vibaya katika kila mechi.
Scholes, ambaye alicheza michezo 714 akiwa ndani ya kikosi hicho, bila kuwataja alisema wachezaji ni mzigo mkubwa kwa Manchester United kwa sasa.
