LONDON, England
TIMU ya Chelsea wanatazamiwa kufanya mazungumzo zaidi na Manchester United kuhusu winga wa Argentina Alejandro Garnacho, 20, ambaye thamani yake ni pauni milioni 50.
Wakati hayo yakiendelea, Manchester United imewaulizia wachezaji wa Bournemouth na Hungary Milos Kerkez, 21, Wolves na Algeria Rayan Ait-Nouri, 23, na kiungo wa Crystal Palace na Muingereza Tyrick Mitchell, 25, huku kipaumbele cha Ruben Amorim kikiwa kumsajili winga wa kushoto.