

LONDON, England
MABOSI wa Nottingham Forest wanataka kumsajili Matheus Cunha Januari hii, Arsenal pia wameonyesha nia ya kutaka kumsaini mshambuliaji huyo wa Wolves.
Nottingham Forest kwa sasa inamtaka kwa udi na uvumba mshambuliaji huyo wa Wolves na Brazil, Matheus Cunha kuwa shabaha yao kuu ya Januari katika harakati za kufuzu Ligi ya Mabingwa.
Arsenal pia wameonyesha nia ya kutaka kumsajili Cunha mwenye umri wa miaka 25 katika uhamisho wa Januari.