Leo januari 20, 2025 kurugenzi ya mawasiliano ya Raisi ikulu, kupitia taarifa kwa vyombo vya habari imetoa taarifa juu ya idadi ya vifo vya mama na mtoto kupungua nchini hadi idadi ya vifo 104 kwa Kila vizazi hai 100,000.
Taarifa hizo zimetoka kwa Raisi wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu kupitia mkutano na waandishi wa habari uliofanyika ikulu chamino akiwa na mgeni wake kutoka shirika la afya duniani (WHO) DKT. Tedros Ghebreyesus. Ameeleza kuwa juu ya juhudi za serikali katika kuhakikisha wanapumguza vifo vya mama na mtoto zimesaidia kupunguza vifo takribani 452 ambapo awali idadi ya wanaofariki ilikuwa 556 na sasa idadi ikipungua hadi watu 104 kwa Kila vizazi hai 100,000.
Aidha ameeleza katika mkutano huo kwamba idadi ya watoto wa umri chini ya miaka mitano imepungu kutoka asilimia sitini na saba Hadi asilimia arobainina tatu kati ya vizazi hai 1000. Hata hivyo vifo vya watoto wanaozaliwa kabla ya wakati vimepungua kwa Kasi ndogo.
Hali kadhalika Raisi Dkt. Samia ameeleza jitihada za serikali katika sekta ya afya katika kuboresha miundombinu ya sekta hiyo kwa kujenga mahospitali kuongeza vifaa tiba imewezeaha asilimia sabini ya wananchi kuweza kupata huduma ya afya ya msingi ndani ya umbali wa kilomita tano.
Lakini pia aliendelea kwa kueleza kuwa 2024 Tanzania ilipiga hatua muhimu katika kuhakikisha huduma za afya zinapatikana kwa watu wote kwa kuzindua mpango jumuishi na shirikishi kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii utakao wafikishia wananchi huduma za kinga, tiba na elimu ya afya mahali walipo bila vikwazo.